DC Kessy Aongoza Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Robo ya Kwanza
“Mama akiwa na mimba ya siku moja, lazima tuanze kumtengeneza ili mama na mtoto wasipate udumavu”.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy, alipokuwa anafungua kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Wilaya kwa Robo ya Kwanza (Julai – Septemba). Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 15, 2023 katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Ihemi Kata ya Mgama.
Mheshimiwa Kessy ameongeza kusema kuwa, Rais wa Awamu ya Sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema Mikoa yote yenye udumavu ijitathamini. Hii ni kutokana na Mkoa wa Iringa kuwa na wadumuvu.
“Tunatakiwa kuwa wabunifu katika suala la kutokomeza udumavu, kwani akina mama tunakaa na watoto muda mwingi hivyo tunawajibika katika malezi na makuzi ya mtoto”. Mkoa wa Iringa haustahili kuwa na udumavu kutokana na wananchi wake kuzalisha vyakula mbalimbali na matunda kwa wingi sana”.
Mheshimiwa Kessy amegusia suala la unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kwa mama mjamzito pia sababu kubwa inayochangua udumavu.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Kessy ametoa agizo kwa Watendaji wa Kata wote kuwa, kila Mtendaji atengeneze shamba darasa, na kushirikisha wananchi ili waje wajifunze hapo, na kila mmoja achukue hatu ili kuleta matokeo chanya.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa amesema, Watendaji wasijitetee kuhusu utafiti unaofanywa na Sekta binafsi, wanatakiwa wafanye kazi bila kuangalia nani kafanya nini. Pia amewatia moyo kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwahimiza Watendaji hao waendelee kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya udumavu, kwani kuna baadhi ya changamoto haziepukiki.
Akitoa taarifa ya Kadi Alama ya utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa Lishe Ngazi ya Wilaya kwa kipindi cha Julai –Septemba Afisa Lishe Wilaya Bi. Tiliza Mbulla amesema “lishe imeendelea kujadiliwa kwa kuzingatia mkakati wa lishe wa Kitaifa ili kuweza kufanikisha matokeo tarajiwa, kupunguza lishe duni, kupunguza ukosefu wa virutubishi, kupunguza uzito uliozidi na uliokithiri na kuweka mazingira wezeshi ya lishe. Hivyo ili kuhakikisha matokeo tarajiwa yanafikiwa utekelezaji unafanyika na kupimwa kuptia viashiria vya mkataba wa lishe”.
Bi. Tiliza ameendelea kusema, utekelezaji wa utoaji wa chakula shuleni unaoratibiwa na Watendaji wa Kata umeendelea kuimarika ambpo Kata moya ya Ilolompya ndiyo yenye idadi ndogo ya wananfunzi wanaopta walau mlo mmoja.
Aidha, katika kiashiria cha kiasi cha fedha zilizotumika kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka mitano katika Halmashauri (Tsh. 1,000.00) na asilimia ya fedha zilizotumika kutekeleza shughuli za lishe zilitolewa kwa asilimia 106 kulingana na mpango. Pia wazazi na walezi waliohudhuriia kliniki ya afya ya uzazi na mtoto walipata elimu ya ulishaji wa watoto wachanga na wadogo ambapo ilifikiwa kwa asilimia 100.
Bi. Tiliza ameendelea kwa kubainisha mafanikio katika kutekeleza viashiria vyote vya Mkataba kwa ufanisi na ongezeko la asilimia 2.0 kwa idadi ya shule zinazotekeleza mpango wa utoaji chakula shuleni.
Pia changamoto ya uchangiaji usioridhisha wa chakula kwa wananfunzi pamoja na kutopatikana kwa vyakula vilivyoongezwa virutubisho, na kuweza kutatua changamoto hiyo kwa kuendelea kutumia majukwaa mbalimbali kuelimsha jamii juu ya umuhimu wa uchangiaji chakula, na kuanzisha mashamba ya shule.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa