Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica kessy amezindua Kampeni ya chanjo ya surua na rubella katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mapema Februari 15, 2024. Uzinduzi huu umefanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo ambapo umehusisha Halmashauri mbili yaani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Manisapaa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Kessy amesema kuwa waratibu waende wakahakikishe kwamba walengwa wote wakafikiwe kikamilifu kwa siku zilizopangwa.
Naye Mratibu wa Huduma za Chanjo Ndugu Sospeter Tiyara amesema, Surua na Rubella ni magonjwa yanayoweza kukingwa kwa chanjo. Ameongeza kuwa, Magonjwa haya husababisha madhara makubwa kwa afya za Watoto walio na umri chini ya miaka mitano hata vifo.
Kampeni hii inaanza rasmi Januari 15, hadi Februari 18, 2024 na itahusisha watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi miaka mitano (5).
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa