DC Kheri Akagua Miradi Tarafa ya Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James amefanya ziara Agosti 13, 2024 kwa kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Tarafa hiyo.
Akizungumza na Wakandarasi wanaojenga skimu ya umwagiliaji Mhe. Kheri ameona mapungufu katika mradi huo wa kuchelewa kukamilika, kwani muda waliopangiwa kukamilisha mradi huo ulishapita. Wakandarasi hao wamesema sababu za kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na ucheleweshwaji wa malipo kutoka Serikali Kuu.
Mhe. Kheri pia aliweza kutembelea Hospitali ya Wilaya iliyopo Igodikafu na kujionea huduma zitolewazo. Akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dr. Godfrey Shirima amesema, “ huduma zinazotolewa kwa sasa ni wagonjwa wa nje (OPD), meno, maabara, mionzi na upasuaji akina mama wajawazito”. Ameongeza kusema kuwa, huduma ambazo bado kukamilika ni kama chumba cha kuhifadhi maiti, kulaza watoto, wagonjwa wa dharura japo kuwa majengo yapo yamekamilika isipokuwa vifaa tu. Mhe. Kheri ameridhishwa na huduma hizo kwani asilimia kubwa ni huduma muhimu na kuahidi kufuatilia vifaa hivyo ili kuongeza huduma kwa wananchi.
Watumishi wa hospitali hiyo wameiomba Serikali kujengewa nyumba za watumishi, na uzio wa hospitali.
Mhe. Kheri amepata nafasi ya kutembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na kuweza kuongea na watumishi. Mkuu wa Chuo hicho Bi. Petronia Shata amesema, kwa sasa chuo kinatoa mafunzo ya muda mrefu kwa kozi za ujenzi, Uashi na ushonaji ambapo kuna wanafunzi 67 ikiwa wasichana 20 na wavulana 47. Pia katika kozi za muda mfupi kama udereva, computer, umeme, magari na ushanaji na kwamba kwa sasa kuna wananfunzi 45 ikiwa wasichana 5 na wavulana 40.
Bi. Petronia ameweza kutaja changamoto zinazowakabili kama maji, umeme kukata mara kwa mara, mazingira, uzio na vifaa vya kujifunzia. Mhe. Kheri ameyachukua na kuahidi kufanyia kazi.
Kadhalika Mhe. Kheri amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuleta watoto waje wajifunze fani mbalimbali, kwani chuo hicho kimejengwa kwa ajili yao.
Pia Mhe. Kheri ameweza kufika hadi katika Kijiji cha Kinyika Kata ya Mlenge eneo ambapo itajengwa shule mpya ya msingi. Eneo hilo limetolewa na wananchi wenye nia njema ya kuiunga mkono Serikali na kuleta maendeleo. Ujenzi utaanza mara moja na mkandarasi amepewa miezi mitatu hadi kukamilika kwa ujenzi huo.
Mhe. Kheri amepata nafasi ya kuongea na wananchi wa Kijiji hicho kwa niaba ya Tarafa ya Pawaga, na kuwapongeza Mbunge, Madiwani na viongozi wote wa Kata hizo kwa kazi nzuri wanazofanya.
Amepongeza juhudi hizo kwa kuleta maendeleo katika miundombinu ya shule, afya na miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa katika Tarafa hiyo, na kuwaomba wananchi wasichoke kutoa ushirikiano katika miradi ya maendeleo inayoletwa na kutoa nguvu kazi zao kwa kuchangia maendeleo.
Wananchi nao waliweza kutoa kero zao zikiwepo za upande wa elimu, afya na maji. Mhe. Kheri aliweza kuzipokea na kuzitatu hapo hapo, kutoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji katika kufanikisha mahitaji ya wananchi, ikiwa ni Afisa Biashara, Afisa Maendeleo ya Jamii waweze kwenda kijijini hapo kutoa elemu ya jinsi ya kufanya biashara na kujiwekea akiba, kutatua mgogoro wa mipaka kati ya Kijiji cha Isele na Kinyika, kuleta Mhuduma wa Afya katika Zahanati ya Kinyika.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa