DC Moyo Aitaka Kamati ya Lishe IDC Kuhakikisha Inaandaa Bajeti ya Lishe Iliyojitosheleza
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amewataka Wajumbe wa Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kutenga bajeti ambayo itakuwa imezingatia makundi maalumu ya walengwa na kuhakikisha ina akisi uhalisia.
Amesema fedha hizo zitengwe kulingana na shughuli husika zinazokadiriwa kufanywa aidha amesisitiza pia kutenga mafungu kwa ajili ya watendaji ambao watakwenda kutekeleza na kusimamia shughuli za lishe katika vijiji basi nao wazingatiwe.
Ameyasema hayo mapema leo 19 Novemba, 2022 alipokua akifungua kikao cha kujadili maandalizi ya makisio ya bajeti ya lishe kwa mwaka 2023/2024. Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri (Siasa ni Kilimo).
"Hata kama kuna kamati ya hamasa ambayo ipo kwa lengo la kuhamasisha nayo msiisahau katika mipango, Muhakikishe hamumsahau mtu au kamati yoyote ili katika utekelezaji msikumbane na changamoto yoyote". Ameongeza.
Naye Afisa Lishe Mkoa Bibi Neema Mtekwa Amesema kuwa suala la lishe bora ni suala endelevu lazima kuwepo na muendelezo na amesema pia lishe ni chakula hivyo lishe bila chakula haiwezekani amesisitiza kwa Wataalamu kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa wananchi juu ya umuhimu wa lishe bora na athari za kutokua na lishe bora.
"Kila kaya lazima iwe na chakula cha kutosha yani wale washibe, hata kama ni maskini natarajia hapa wataalamu watawasaidia kuwajengea uwezo wa kimkakati wa namna ya kupata kipato na kukitunza kile wanachokipata".
Aidha kwa kufanya vikao vya tathmini kuona wanawasaidiaje hawa watu aidha kwa kuwaingiza katika vikundi vya ujasiriamali au hata shughuli hizo hizo za kilimo lakini kuwapa mbinu za namna ya kujikwamua kiuchumi ili mwisho waweze kumudu gharama za chakula. Ameongeza.
Bibi Mtekwa pia amezungumza kuhusu suala la matumizi sahihi ya fedha za lishe kwa kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliowekwa ili kuepuka kuibuka kwa hoja pindi wakaguzi wanapokuja kuhakiki na kuwataka wajumbe kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha matumizi ya fedha za lishe hayatumiki tofauti na ilivyopangwa.
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya Bibi Tiliza Mbulla Amesema kwa bajeti iloyopita ilitumika vizuri na ilileta mafanikio chanya na bajeti iliyokua imetengwa ilikua ni Tshs. 62,830,000 kiasi kilichotumika ni Tshs 56,188,150 Sawa na asilimia 89.4 huku Mkurugenzi Mtendaji akiidhinisha 96.8% ya fedha iliyotengwa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri , hivyo amemshukuru sana.
Akifunga kikao hicho Katibu Tawala Wilaya ya Iringa Ndugu Estomin Kyando amewashukuru wajumbe wote waliohudhuria na kusisitiza juu ya yale yaliyopendekezwa kutumika inavyotakiwa ili suala la udumavu liweze kukomeshwa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa