DC Moyo Awataka Wananchi Kuacha Kunung’unika
Mkuu waa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohammed Moyo amesema taifa haliwezi kupiga hatua za kimaendeleo ikiwa Watanzania bado tutaendelea kunung’unika na kunyoosheana vidole ni lazima kufanya kazi kwa bidii.
Amesema Mataifa yote yaliyoendelea duniani watu wake walifanya kazi na hakukuwa na mtu yoyote aliyetoka nje yao kwenda kuwasaidia katika maendeleo yao, hivyo ili kuendelea kuijenga Tanzania yetu bora na imara ni lazima kufanya kazi kwa bidi.
Ameyasema hayo mapema katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyoadhimishwa kiwilaya tarehe 09.12.2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ulipofanyika mdahalo maalumu wa kujadili maendeleo ambayo nchin yetu Tanzania imefikia na kujadili kwa pamoja tulikotoka, tulipo na tuendako
“kwa sasa tunajitawala wenyewe hivyo kila Mtanzania ni lazima ajivunie hilo na tuendelee kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa bidii, Hakuna njia ya mkato ndugu zangu watanzania ni lazima tuchape kazi kwa sababu nguvu tunazo, uwezo tunao hivyo taifa hili litapata maendeleo kama sisi wenyewe tutachapa kazi”.
Amesema pia miaka hii 61 ya Uhuru haikuwa rahisi kwani wazee wetu walijitoa maisha yao, nguvu zao, mali zao mpka kupatikana kwa uhuru wetu, hivyo amesema kwa watanzania ambao wamezaliwa baada ya uhuru kuendelea kuuenzi uhuru na amani yetu ambayo tumekuwa nayo kwa kipindi cha miaka 61.
“Tuendelee kuulinda uhuru wetu, tuendelee kulinda na kudumisha mafanikio yetu yote ambayo Tanzania imeyapata kuanzia kwa viongozi wetu waliopita na viongozi wetu wajao wanaotaka tuyafikie, huo ndio itakuwa uzalendo wa kweli”.
Aidha amesema sisi kama taifa ni lazima tuwe na msimamo wetu na mipango yetu ya kufanya kama taifa hususani uapande wa maadili kwani kwa siku za hivi karibuni maadili yameonekana kuporomoka kwa kiasi kikubwa hususani kupitia mitandao ya kijamii, hivyo ameagiza kurejea kwenye tamaduni zetu tulizolelewa nazo.
Pis Mhe. Moyo ametumia Jukwaa hilo kutoa rai kwa wananchi juu ya Kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuendelea kukemea na kutoa taarifa za ukatili zinapotokea au kuonekanapo kwa dalili za ukatili. Ameongeza kwa kusema kuwa Iringa bila Ukatili inawezekana na ni lazima tushinde vita hiyo.
Mdahalo huo umehusisha Watumishi wa Umma wote kutoka Halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Iringa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Vyama vya Siasa, Viongoziu wa Dini, baadhi ya Wahadhiri na Wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Iringa na Shule za Msinga na Sekondari, Viongozi wa makundi mbalimbali pamoja na wananchi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa