Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndg. Robert Masunya ameongea na watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri yaliyopo kijiji cha Ihemi kuhusu masuala mbalimbali ya kazi na kiutumishi Julai 23, 2024.
Ndugu Masunya amesisitiza juu ya utii wa sharia kwa kila mtumishi na kwamba kuwahi kazini na kila mtumishi kutimiza wajibu wake wa kazi kwa wakati ni sharia.
Aidha ametahadharisha juu ya suala la rushwa kwa watumishi wakati wa utoaji huduma na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, “Rushwa imezuiliwa kwani huharibu usimamiaji imara wa miradi yetu na kufifisha mwenendo mzima wa ufanyaji kazi wa watu waliopewa dhamana ya kusimamia kazi, matokeo yake ni kwamba miradi haiishi na kukosa ubora” amesema
Amesongeza kusema, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepokea fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zaidi ya Bilioni 6 hivyo usimamizi thabiti unahitajika ili fedha zilizoletwa zikatoe matokeo yaliyotarajiwa na jukumu hilo ni la kila mmoja wetu ndio sababu tunapaswa kujua kinachoendelea.
Kwa upande wa Afya ndugu Masunya amewaasa watumishi kujitunza na kujilinda na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuwakumbusha watumishi wawe na kawaida ya kupima afya zao ili waweze kuchukua hatua na tahadhari zingine. Ameongeza kuwa kwa watumishi wapya hasa ajira mpya ni mhimu wakachukua muda kujifunza mazingira kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri wamempongeza Mkurugenzi kwa kuwa na kikao hicho na kukumbusha baadhi ya masuala yanayowasibu ikiwemo stahiki za watumishi za uhamisho kutoka Iringa Mjini hadi kijiji cha Ihemi yalipo makao makuu ya Halmashauri jambo linalosababisha kuwa na maisha magumu ya utendaji kazi. Suala hili Mkurugenzi ameahidi kulichukuwa na kuwakumbusha watumishi kuishi kwa upendo na hivyo kutoa huduma nzuri kwa wateja wanaowahudumia.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa