Dkt. Biteko Azindua SHIMIWI Iringa
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amewataka wanamichezo kutumia nafasi zao katika kutangaza viuti vya Utalii ndani na nje ya Nchi, na kulinda mazingira kwa kuwaelekeza watu umuhimu wa utunzaji mazingira.
Mheshimiwa Dkt. Biteko ameyasema hayo Oktoba 04, 2023 katika viwanja vya Samora Mkoani Iringa wakati akifungua Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), ambapo amewataka washiriki wa michezo hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya talii vilivyopo nchini Tanzania, ili kukuza uchumi, na kupelekea Sekta ya Utalii kukua kwa kasi kubwa.
Aidha Mhe. Dkt. Biteko amewasisitiza wanamichezo hao kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti, kulinda vyanzo vya maji.
Nae Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mheshimiwa Patrobas Katabi (Mb), ametoa shukrani kwa Serikali kwa kuanzisha mashindano hayo, ambapo hii ni michezo ya 37 tangu kuanzishwa kwake, huku Watumishi 2765 wameshiriki katika michezo hiyo vikiwemo Vilabu 68 kwa mwaka huu.
Akitoa taarifa ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiw Halima Omary Dendego, ameishukuru Serikali kwa kazi kubwa inayofanya katika Mkoa huo kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo. Pia kwa kuruhusu mwaka huu mashindano ya SHIMIWI kufanyika Mkoani Iringa, kwani mashindano haya yamechangia na kuongeza uchumi ndani ya Mkoa.
Mashindano hayo ya SHIMIWI yanatarajiwa kufungwa Oktoba 14, 2023.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa