DSW Yatambulisha Mradi wa REST
Shirika lisilo la Kiserikali la Deutsche Stiftung Wettbevolkerung – DSW kwa kushirikiana na Mashirika ya TAHEA na Alama Yangu za Mkoani Iringa, wametambulisha mradi wa Reproductive Equity Strategy in Tanzania - REST, ambao utajikita katika kuhudumia vijana wa rika mbalimbali katika masuala ya uzazi na uchumi. Hafla ya utambulisho wa Mradi huo imefanyika Novemba 15, 2024 katika Ukumbi wa Hotel ya Sun Set iliyopo Manispaa ya Iringa.
Shirika la DSW lilisajiriwa mwaka 2006 na Makao yake Makuu yapo Arusha, lenye lengo la kutoa elimu ya afya na maendeleo katika nyanja ya uchumu kwa vijana.
Katika kuanza kwake kufanya kazi Shirika la DSW lilianza kazi katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, na sasa wameingia Mbeya, Songwe na Iringa. Katika Mkoa wa Iringa Shirika litafanya kazi katika Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Shirika litashirikiana na TAHEA na kuafanya kazi katika Kata Nne ambazo zina changamoto nyingi kwenye eneo la vijana ambazo ni Ifunda, Mseke, Kising’a na Kihorogota.
Akizungumza katika utambulisho wa mradi huo Mkurugenzi wa Shirika la DSW Ndugu Peter Owaga amesema, lengo la Shirika ni kutoa mafunzo kwa vijana juu ya stadi za maisha, elimu ya uzazi, kutokomeza ukatili, kuwajengea uwezo wa kujitegemea na ujasiriamali, kujikinga na VVU, mimba za utotoni na kuanzisha vikundi mbalimbali, kwa vijana.
Baada ya kuwafikia walengwa Shirika la DSW linatarajia kuona kuimarika kwa ushiriki, kuongezeka kwa uwezo wa Wadau, kuanzisha kwa Klabu za Afya shuleni, kuwezesha vijana Mabalozi na Klabu za Afya.
Ndugu Owaga ameendelea kusema kuwa, vijana ambao watawafikia ni walio ndani na nje ya mfumo wa shule, Vyuo Vikuu na wale wa mtaani.
Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la TAHEA Ndugu Peter Mapunda na Mkurugenzi wa Alama Yangu Bi. Joyce Ernesta wamepokea kwa mikono miwili Shirika la DSW na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuwafikisha katika Kata zote ambazo zimepangwa kutembelewa.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Shirika la DSW litashiriiana na Shirika la TAHEA kama Shirika na mwenyeji na upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa watashirikiana na Shirika la Alama yangu ambapo watafanya kazi katika Kata Tano za Manispaa ambazo ni Makorongoni, Ruaha, Kihesa, Mkwawa na Mtwivila.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa