Mkutano wa Baraza la Madiwani kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali limefanyika Juni 17 likiongzwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba.
Mhe. Serukamba ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata Hati Safi kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 na kuwasisitiza kuwa makini katika ufanyaji wa manunuzi na kuweka rekodi vizuri.
Mhe. Serukamba pia amesisitiza ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo katika bajeti tuliyopanga na kukamilisha hoja zote kila baada ya robo mwaka, na kwamba hoja zote zijibiwe kwenye mfumo kwa wakati.
Aidha, Mhe. Serukamba ametaka madeni yote yaliyotokana na mikopo ya 10% ambayo ni ya muda mrefu yakusanywe na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamesababisha madeni hayo.
Mhe. Serukamba ameendelea kusema, anataka miradi ikamilike kwa wakati ikiwa kila fedha ya mradi imefika kwa wakati na kwa kiasi kinachotakiwa katika kutimiza mradi husika.
Pia amesema Kitengo cha Ukafuzi wa Ndani kipatiwe vifaa ili kiweze kufanya kazi yake kwa uhakika na kwa usahihi.
Maagizo hayo yote yamepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya na kuahidi atayafanyia kazi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa