Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Yazindua Miongozo ya Kuimarisha Sekta ya Elimu
Serikali Wilayani Iringa imezindua rasmi Miongozo ya Elimu Msingi na Sekondari iliyondaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI yenye lengo la kuboresha Sekta muhimu ya Elimu hapa nchini, ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznai Mheshimiwa Kassim Majaliwa kuzindua Miongozo hiyo kwa Ngazi ya Taifa.
Miongozo hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya, ni pamoja muongozo wa uteuzi wa ngazi mbalimbali za viongozi kwa Mmalaka za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa. Miongozo inabainisha mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji kwa Ngazi za Elimu Msingi na Sekondari, wakati muongozo wa tatu ukizingatia kutafuta suluhu ya changamoto katika uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari.
Akitoa hotuba yake katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Mohamed Moyo amesema, “Utoro wa Walimu unaweza kuwa wa aina mbili, yaani kutofika shuleni au kutofundisha vipindi vyake . Athari za utoro wa walimu ni pamoja na kushindwa kumaliza mada kwa wakati na kuwapotezea muda wananfunzi na hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea na masomo. Natoa wito kwa Wakuu wa Shule kusimamia mahudhuria na utendaji wa walimu. Aidha Mamlaka za kinidhamu kwa Walimu zichukue hatua mara moja kwa walimu wnaokwenda kinyume na maadili yao ya kazi ya Ualimu”
Mheshimiwa Moyo ameendelea kusema kuwa, katika changamoto ya utoro wa wanafunzi wadau wote wakiwemo wazazi na wananfunzi wenyewe, washirikiane kwa karibu. Wazazi wana jukumu kubwa la kufuatilia maendeleo ya wanafunzi wao. Aidha natoa wito kwa Watendaji wa Kata na Maafisa Elimu Kata kuhakikisha mnachukua hatua kwa wazazi wote wanaosababisha watoto wao kutohudhuria shule. Hatua hizi ni pamoja na kutekeleza haki ya elimu kwa kila mtoto hivyo kusababisha mtoto kutokwenda shule na kumnyima haki yake'.
Pia changamoto ya ukosefu wa chakula Shuleni na kusababisha wazazi wengi kukataa kuchangia chakula, baadhi ya wazazi kutouamini uongozi wa shule katika kupokea chakula kwa kuhofia chakula hicho kutumiwa na walimu na familia zao na baadhi ya walimu kutoona umuhimu wa kuwa na shamba la shule. Vilevile uongozi wa shule kushindwa kusimamia ufundishaji na upimaji.
Baada ya maelezo hayo Mheshimiwa Moyo ametoa maelekezo yafuatayo ikiwemo, kila uongozi katika ngazi zote kuhakikisha unakuwa na miongozi hii kama dira katika kutatua changamoto, Wakuu wa Shule na Walimu wote wanaipitia miongozo hii na kuweka mikakati na mpango kazi wa kutatua changamoto zote katika shule.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Beatirice Augustine alikuwa na haya ya kusema, “Leo hii tunafanya Uzinduzi wa Miongozo hii Mitatu ambayo ni maelekezo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyoizindua hivi karibuni. Lengo kuu ni kuleta Mapinduzi katika Sekta ya Elimu kwa kuimarisha usimamizi na utoaji wa elimu bora nchini”.
BI. Beatirice ameendelea kusema kuwa, “Halmashauri yetu imekuwa ikifanya vizuri katika elimu kwa ngazi ya Mkoa na hata Kitaifa, hivyo uzinduzi wa Miongozo hii utaongeza ufaulu na ubora wa elimu kwani miongozo hii itatupatia nyenzo za kutendea kazi kwa watandaji katika ngazi zote pamoja na wadau wa elimu”.
Aidha ameongeza kusema, “mimi kama Msimamizi Mkuu wa Halmashauri kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani, pamoja na wadau mbalimbali wa elimu, tunaahidi kuisoma, kuielewa na kutekeleza maelekezo yote yaliyobainishwa katika miongozo hii kwa lengo la kupata viongozi bora wa kielimu wanaoweza kusimamia na kutoa majawabu ya changamoto mbalimbali katika Sekta ya Elimu.
Aidha Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Ndugu Sylvester Mwenekitete amepata nafasi ya kutoa ufafanuzi katika uzinduzi wa miongozo hiyo na kusema, “muongozo wa kwanza ni changamoto katika uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari ni kuwa, kitabu kimebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na pia hatua za kuchukua kwa kila changamoto. Baadhi ya changamoto ni, upungufu wa miundombinu, utoro wa wanafunzi, baadhi ya wanafunzi kutomudu satadi za KKK, utoro wa Walimu, Upungufu wa Walimu, ukosefu wa chakula shuleni, na umbali kati ya shule na makazi ya watu”.
Mwenekitete ameendelea kusema, Muongozo wa pili ni Mkakati wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu Msingi, na kufafanua kuwa, lengo la elimu ni kumkomboa Mtanzania kutoka katika hali duni kimaisha na kiuchumi, pia hali ya elimu ya msingi na sekondari nchini na mikakati thabiti ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji. Aidha muongozo unaonesha namna ya usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya mikakati pamoja na kusisitiza ushiriki wa wadau, wazazi na wanafunzi katika kutekeleza mikakati.
Mwenekitete amemaliza kwa kusema Muongozo wa tatu ambao unataja Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa kwamba maendeleo ya kielimu katika ngazi zote yanategemeana sana na sifa za kiongozi, kwani kiongozi katika ngazi ya shule na kata ni nguzo muhimu sana kusimamia ufundishaji wa walimu na ujifunzaji wa wanafunzi. Pia muongozo umebainisha sifa za viongozi na kamati zinazopaswa kufanya uteuzi wa viongozi hawa katika ngazi zote. Kabla ya muongozo huu uteuzi wa viongozi wakiwemo Wakuu wa Shule na Maafisa Elimu Kata ulikuwa ukifanywa na kamati ya watu wachache na kupelekea kuwapata baadhi ya viongozi ambao wameshndwa kuleta mabadiliko ya elimu kama ilivyotarajiwa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa