Hamashauri ya Wilaya ya Iringa Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka USAID - Jifunze Uelewa kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum
Msaada huo wa vifaa vya kujifunzia umetolewa leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wa Siasa Ni Kilimo.
Akikabidhi vifaa hivyo Ndugu Japhari Shehaghilo, Afisa Elimu Jumuishi na Uhamasishaji Jamii Mradi wa USAID- Jifunze Uelewa amesema, “watu wenye elemavu nao pia wana haki ya kujifunza, kupata burudani na kushirikishwa na jamii, hivyo si vizuri kuwatenga. Sisi kama Shirika la USAID tumeona ni vema sasa tuwapatie watoto hawa Runinga na vifaa vingine ili nao waweze kujifunza na kupata burudani”.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Runinga mbili (smart tv inch 43), kompyuta mpakato tatu (Laptop 3), Orbit reader 2 (kifaa cha kuandikia na kusomea chenye memory card).
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Halmashauri Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Steven Mhapa amesema, “kwanza tunashukuru kwa Shirika hili la USAID kwa kutoa vifaa hivi kwa ajili ya watoto wetu, na naomba kuendelea na moyo huo wa kujitolea hata kwa mambo mengine”.
Mheshimiwa Mhapa ameongeza kusema kuwa, si vizuri kwa wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu. Tuwatoe na kuwapeleka shule ili nao wakajifunze, pia ni haki yao kupata elimu na kuchangama na jamii.
Vifaa hivi vitapelekwa kwa shule ya Msingi Kipera na Tanangozi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa