Ibo Italia Wakabidhi Chumba cha Upimaji
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Joseph Kinyanyah Mei 28, 2024 amepokea jengo la kupmia wanafunzi wenye mahitaji maalum kama uoni, ulemavu wa viungo, akili na usikivu lililojengwa na Shirika la Ibo Italia ambapo jengo hilo linaitwa “Chumba Chetu” katika Shule ya Msingi Kipera.
Akitoa ahadi kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Paola Ghezzi Kinyanyah amesema jengo hili litasaidia kujua mtoto ana shida na njia ipi itumike kumsaidia, pia litasaidia kwa shule zingine zenye mahitaji maalum kama Tanangozi, Kidamali na Mfyome zote hizi zitaenda kunufaika na mradi wa Chukba chetu.
Aidha, Kinyanyah amewaambia wazazi kuwa mtoto ana fursa za kusoma bila kujali hali yake, huku akiowaomba wazazi kuwa mabalozi kwa wazazi wengine, ili kuongeza idadi ya watoto wenye mahitaji maalum kupatiwa elimu, kwani mpaka sasa shule hiyo ina watoto 750 tu.
Vilevile amewaambia wazazi hao kuwa washirikiane kwenye miradi ya maendeleo kwani kwani Serikali inatoa pesa lakini inahitaji pia nguvu kazi kutoka kwa wananchi ili kukamilisha miradi hiyo.
Pamoja na hayo Bwana Kinyanyah amewasihi wazazi wawe wanakwenda mara kwa mara kuwatembelea watoto hao na kujionea maendeleo yao.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Paola amesema yote haya yasingewezakana bila kushirikiana vizuri na uongozi wa Halmashauri na shule ya Msingi Kipera. Akisisitiza kuwa Serikali inaweza kusaidia, pamoja na mashirika ila wasisahau kuwa haya ni majukumu ya wote.
Bi. Paola amekabidhi mradi huo uliogharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania 30.2 ambapo utatoa msaada kwa watoto hao.
Naye Afisa Elimu Elimu Maalum Bwana Wilfred Mattu amepongeza na kushukuru Serikali kwa kuruhusu Mashirika kutoa misaada kwa watoto hao na kusema watoto hao wanahitaji fursa kama watoto wengine.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa