Iringa DC Kuimarisha kikosi kazi Usimamzi na Ukusanyaji Mapato
Halmashauri za Mkoa wa Iringa zimekutana kwa lengo la kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa robo ya kwanza (julai hadi septemba) mwaka wa fedha 2022/2023. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa siku mbili tarehe 18 na 19.10.2022.
Katika mwaka wa fedha 2022/23, Halmashauri za Mkoa ziliidhinishiwa kukusanya jumla ya shilingi 26,744,971,245.32 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani (Own Source). Hadi kufikia tarehe 30 septemba, 2022 jumla shilingi 5,141,808,845.32 zilikuwa zimekusanywa sawa na asilimia 19.22 ya lengo.
Mchanganuo wa makusanyo ya ndani kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 julai, 2022 hadi tarehe 30 septemba, 2022 bajeti iliyoidhinishwa ni Tshs. 4,269,100,000.32 na makusanyo hadi kufikia tarehe 30 septemba 2022 ni 720,321,648.00 na jumla ya asilimia ya makusanyo ni 17.00.
Akiwasilisha mafanikio yaliyopatikana wakati wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa robo ya kwanza mwaka wa fedha 2022/2023 Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Fredy Kaduma amesema wamefanikiwa kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni nyumba mbili (2) apartment za kupangisha, ushuru wa maegesho wa magari na ushuru wa stendi ya basi - Migoli.
Kwa upande wa changamoto Kaduma amesema Halmashauri imekumbana na changamoto ya ukosefu wa soko la ununuzi wa zao la tumbaku, wakulima wameacha kuzalisha na hivyo Halmashauri kukosa mapato kwenye ushuru huu. Kadhalika kushuka kwa uzalishaji wa samaki katika bwawa la samaki la Mtera limeathiri kiwango cha ukusanyaji mapato.
Utambulisho wa vitambulisho vya Ujasiriamali pia vimepunguza mapato yaliyokuwa yakikusanywa kwenye baadhi ya vyanzo ambavyo Halmashauri inavitegemea kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye bajeti ya mapato ya ndani ikiwa ni eneo la makusanyo ya ushuru wa mazao/mbogamboga na matunda. Ameongeza.
Amesema hatua zilizochukuliwa na Halmashauri kukabiliana na changamoto hizo ni pamoja na Halmashauri imeandaa mfumo wa kanzidata (database) ili kuorodhesha walipa kodi wote wa ushuru mbalimbali wa Halmashauri kadhalika na kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki na kuimarisha kikosi kazi cha kusimamia na kukusanya mapato ya Halmashauri.
“Halmashauri pia imeendelea kufanya mawasiliano na wanunuzi wakubwa wa zao la tumbaku na kutataua changamoto zinazozikabili vyama vya msingi ili waweze kulima tena na Halmashauri ikusanye mapato.”
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa, Sehemu ya Mipango na Uratibu Ndugu Kasongwa Owden amesisitiza juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa kama makisio ya ukusanyaji wa mapato.
Naye Muweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bibi Jwani M. Yengi amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha ukusanyaji wa mapato lakini nyingi katuika hizo zinafanyiwa kazi
“Tunatarajia kuingiza kiasi cha Tshs. Milioni 400 kutoka katika chanzo cha uuzaji wa viwanja ili kufikia lengo tumeanza uhamasishaji kwa njia mbalimbali ikiwemo matangazo lakini pia tunatarajia kupunguza bei ili tuweze kufikia lengo lililowekwa”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa