Iringa DC Wapanda Miti Kuenzi Miaka 61 ya Uhuru
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameshiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo zoezi ka upandaji miti katika Shule ya Msingi Kalenga na Shule ya Msingi Isakalilo kama sehemu ya kuenzi miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katika shughuli hizo ya upandaji miti Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa (DAS), Estomin Kyando aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Mohammed Moyo amesema shughuli hizo zinaendelea katika kata mbalimbali.
Hayo yamefanyika tarehe 07.12.2022, Ikiwa ni kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kwa mwaka huu Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yafanyike Kiwilaya huku kukiwa na Midahalo na Makongamano mbalimbali kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia.
Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa