Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imefanya maadhimisho ya Juma la elimu ya watu wazima Septemba 03, 2025 katika viwanja vya Mahakama kijiji cha Migoli tarafa ya Ismani.
Maadhimisho haya yamefanyika Iringa DC kimkoa ambapo kumekuwa na ushiriki wa wadau mbalimbali wa elimu ya watu wazima (MEMKWA & MKEJA) wakiwemo wanufaika wa program hii waliojiunga na masomo kwa nuia hii na wengine wajasiriamali waliowezeshwa kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika Juma la Elimu ya watu wazima Mwl. Rejinaldo Msendekwa Afisa Taaluma Mkoa ametembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa kupitia program za elimu ya watu wazima (MEMKWA & MKEJA) katika viwanja vya mahakamani kijiji cha Migoli kabla ya kuzungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Maadhimisho ya mwaka huu yamepambwa na kaulimbiu isemayo, "Kukuza kisomo katika zama hizi za kidijitali kwa maendeleo endelevu ya Taifa ketu"
#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa