Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Yafanya Ziara Kukagua Miradi ya Maendeleo
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Kamati hiyo imefanya ziara Mei 13, 2024 na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa mwaka huu wa fedha ambapo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa na matundu 8 ya vyoo katika shule ya Sekondari Kiwele Kata ya Kiwele. Ujenzi wa vyumba vya madarasa umetumia kiasi cha Shilingi Milioni 104, na ujenzi wa vyoo umetumia Shilingi Milioni 16 na kuleta jumla ya fedha zote za mradi kiasi cha Shilingi Milioni 120.
Ujenzi huo ulianza Aprili 05, 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2024. Hatua ya ujenzi imefikia 85%. Wajumbe wametoa pongezi kwa Kamati ya ujenzi kwa usimamizi mzuri wa mradi.
Katika mradi wa ujenzi wa vyoo matundu 16 Shule ya Msingi Kiwele, ujenzi umeendelea vizuri na kiasi cha Shilingi Milioni 46.7 kilitolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo hivyo. Ujenzi umefikia 45%, na wajumbe walimuagiza fundi aongeze kasi ya ujenzi ili kuendana na muda. Ujenzi ulianza Aprili 15, 2024 na unategemewa kukamilika Juni 30, 2024.
Kata ya Ilolompya kuna ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Ukwega. Kiasi cha Shilingi 100 kiliolewa kwa ajili ya ujenzi huo na sasa ujenzi umefikia 10%. Ujenzi ulianza Aprili 17, 2024. Ujenzi ulichelewa kuanza kutokana na sababu za ucheleweshwaji wa vifaa, hivyo Kamati imemuagiza fundi kuharakiksha ujenzi huo ili kufikia lengo.
Shule ya Sekondari Pawaga Kata ya Itunundu kuna ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 8 vya vyoo, ambapo kiasi cha Shilingi 164 zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo wa madarasa na vyoo. Ujenzi ulianza Mei 2, na unatarajiwa kukamilika Juni 2024, na kwamba ujenzi umefikia 10%. Mradi huu umechelewa kuanza kwa sababu zinazosemekana kwa kuchelewa kwa madini ujenzi kutopatikana kwa wakati. Kamati imesisitiza fundi aharakishe ujenzi ili kuendana na muda.
Kata ya Mlenge katika Kijiji cha Isele kuna ujenzi wa Kituo cha Afya, ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 329 zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Ujenzi ulianza Aprili 25, na unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2024. Hadi sasa ujenzi umefikia 10%. Kamati imemuagiza fundi kuharakisha ujenzi kwani vifaa vyote vipo eneo la ujenzi.
Katika kutekeleza miradi yote ya maendeleo, wananchi wanatakiwa kushikishwa kwa kila hatua ili waweze kuchangia ujenzi. Wananchi wamekubali kuchangia maendeleo na kuomba kupatiwa risiti mara wanapochangia michango mbalimbali ya maendeleo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa