Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maji na Mazingira Wakiwa Magulilwa, Luhota na Masaka
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maji na Mazingira imeweza kuendelea na ziara ya kukagua miradi ya maji kwa siku ya Pili katika Kata ya Magulilwa, Luhota na Masaka Machi 14, 2024.
Mradi wa Maji katika Kata ya Magulilwa katika Kijiji cha Mlanda Kamati imempongeza kwa Mwananchi aliyetoa eneo hilo bure kwa ajili ya kujenga mradi huo. Mradi umekamilika na umeanza kutumika kwa wananchi zaidi ya 9,000 wananufaika.
Naye Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mary Prisca Mahundi ameiambia Kamati kuwa zile fedha zilizoletwa ni kwa ajili ya miradi hii ambayo imeonekana hapo, na kuishukuru Kamati kwa kuja kukagua.
Naye Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya amewaomba wananchi wautunze mradi ikiwa na kulinda vyanzo vya mito visiharibiwe kwa kufanya shughuli za kibinadamu, kwani hii ni Agenda ya Kitaifa ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.
Aidha, Mhandisi Exaud Humbo amebainisha kuwa mradi umetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 1.47 ambapo mradi ulianza Januari 2023 na kumalizika Januari 2024 na mradi unatumika.
Kadhalika katika Kata ya Luhota Kijiji cha Nyabula, mradi wa maji umeweza kukamilika na kuanza kutumika na kwamba utaweza kuhudumia wananchi zaidi ya 1,000 wa Kata hiyo na vijiji jirani.
Katika Kata ya Masaka inayounganisha Vijiji va Makota, Sadani na Kaning’ombe, Kamati iliweza kukagua mradi wa ujenzi wa Bwawa la Maji ambalo limepandwa samaki zaidi ya 12,000. Bwawa hilo litasaidia wananchi kufanya shughuli za umwagiliaji wa mazao mbalimbali.
Kamati ilitoa maoni kuwa, bwawa lijengewe kingo ili kuepusha mmomonyoko wa udongo ambao utaweza kujaa kwenye bwawa.
Naye Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Mathew Nganyagwa aliweza kuwasilisha ombi la kulipwa fidia kwa wananchi waliotoa eneo la nyongeza kwa ajili upanuzi wa bwawa hilo, kwani ardhi iliyotolewa mwanzo walitoa bure.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa