Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maji na Mazingira Yaridhishwa na Uhifadhi Misitu
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maji na Mazingira imeridhishwa na Uhifadhi Misitu na Mazingira ambayo imefanywa na Kata ya Nzihi Kijiji cha Ilalasimba na Magubike, walipotembelea na kukagua mradi huo Machi 13, 2024.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mheshimiwa Jackson Kiswaga imefurahishwa na namna mradi huo ulivyotunzwa na kuleta muonekana na hewa nzuri, ambapo baada ya muda wanavijiji hao wataweza kufanya biashara ya hewa ukaa ambayo kwa sasa ni biashara kubwa duniani kote.
Waziri mwenye dhamana kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mheshimiwa Suleiman Jaffo aliweza kuwongoza Kamati hiyo kuingia msituni na kukagua kama kuna shughuli za binadamu zinafanywa ndani ya msitu huo, lakini walifurahishwa kwa jinsi ulivyotunzwa.
Mheshimiwa Jaffo aliweza kuwafafanulia kuwa msitu huo una Hekta 2,106.3 umeweza kutiririsha maji kutoka kwenye vyanzo vyake ambavyo mwanzo vilikuwa vimekauka kabisa. Pia ufugaji wa nyuki umeanza katika msitu huo ili kuweza kuwaongezea kipato wananchi mara watakapoanza kuvuna asali.
Mheshimiwa Kiswaga amewaasa wananchi wa eneo hilo kutunza msitu huo ili uweze kuwasaidia kuhifadhi mazingira.
Kadhalika katika ufugaji wa ng’ombe wa kikundi cha Israel wamefurahia kutembelewa na Bunge hilo na kuahidi kuongeza ng’ombe ili waweze kupata maziwa ya kutosha na kufanya biashara, ambapo wameweza kuhifadhi mazingira kwa kufugia nyumbani na kulima shamba la nyasi kwa ajili ya mifugo yao.
Kamati imeweza kufika hadi Kijiji cha Itagutwa Kata ya Kiwele ambapo kuna mradi wa maji, uliofanywa na Mamlaka ya Usambazaji wa Maji Vijijini (RUWASA).
Wizara yenye dhamana ambapo Naibu Waziri wake ni Mheshimiwa Mary Prisca Mahundi aliweza kuongoza Kamati kukaga mradi huo na kusema kuwa, mradi utawasaidia wananchi wa Kata hiyo na vijiji jirani kwani tanki lina ujazo wa Lita 200,000 wakati mahitaji ni Lita 100,000.
Kamati imerishwa na mradi huo na kuwaasa wananchi wautunze mradi huo ili uje usaidie kazazi kijacho.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa