Kamati ya Menejimenti ikiongozwa na Mwl. Peter Fussi Afisa Elimu ya Awali na Msingi, akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri, kwa Robo ya Pili kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Baadhi ya miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule ya Msingi Lupembelwasenga iliyopo Kata ya Mgama, ambapo kuna mradi wa ujenzi wa vyoo. Mradi huo umetekelezwa kwa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 42 kwa ajii ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi na walimu matundu 34 ikiwa wavulana matundu 16 na wasichana matundu 16, Walimu matundu 2, pamoja na ujenzi wa mnara wa kuhifadhia tanki la maji.
Mradi ulianza mwaka 2021/2022 na kwamba umekamilikwa kwa 100% na sasa vyoo hivyo vinatumika.
Changamoto iliyopo katika shule hiyo ni uhaba wa maji, hivyo Kamati imeshauri washirikishwe wananchi katika ujenzi matanki ya chini kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua.
Kamati imeendelea na ziara hadi katika shamba la Parachichi lilipo katika Kata hiyo ya Mgama Kijiji cha Ibumila.
Akitoa taarifa ya mradi huo Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bi. Lucy Nyallu amesema, “Kiasi cha Shilingi Milioni 25 kilitengwa kwa ajili ya kulima shamba hilo na kupanda miche ya Parachaichi. Shamba hilo lina ukubwa wa Heka 45, lakini maparachichi yamepandwa kwa Heka 12 tu, ambapo awamu ya kwanza ilipandwa miche 600 na sasa hivi miche hiyo ina miaka mitatu na imeanza kutoa matunda. Awamu ya pili ilipandwa miche 350 ina mwaka mmoja”.
Kamati imeshauri shamba liwekewe uzio kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
Katika Kata hiyo pia Kamati imetembelea mradi wa mabwawa manne ya samaki. Akitoa taarifa ya mradi huo Bi. Nyallu amesema, “kilitengwa kiasi cha Shilingi 116,351,200 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Hadi sasa mabwawa manne yamejengwa, jengo la darasa na stoo kwa ajili ya kujifunzia. Mradi ulianza Januari 2023, na unategemewa kukamilika Januari 2024. Hadi sasa mradi umefikia 99%.
Bi. Nyallu amesema, “bwawa moja lina uwezo wa kuchukua vifaranga wanaozaliana 2,400 na wasiozaliana 3,600. Na kwamba hadi kuvuna samaki hawa inachukua miezi 7 – 8. Samaki watakaofugwa hapo ni aina ya pelege ambao wanafafana na sato. Hii ni kutokana na ukubwa wa soko na hali ya hewa”.
Kadhalika Kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa vyoo katika Shule ya Sekondari Lumuli iliyopo Kata ya Lumuli. Ujenzi huu ulichangiwa na wananchi kwa kiasi cha Shilingi Milioni 3,200, na Halmashauri imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 7,390,461 na kufanya jumla ya Shilingi Milioni 10,590,461. Kiasi kilichotumika hadi sasa katika ujenzi huo ni shilingi Milioni 4,823. Ujenzi ulianza Oktoba 2023, na unategemea kukamilika Januari 2024. Ujenzi umefikia 60%, ujenzi unaendelea.
Isitoshe Kamati imefika hadi Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, ambapo kuna mradi wa ujenzi wa bweni.
Mradi huu ulipata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 130 na kwamba ujenzi ulianza Oktoba 2023 na unategemea kukamilika Januari 20, 2024, maradi umefikia 70%. Bweni lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 80.
Kamati imeshauri fundi aongeze kasi ya ujenzi kwani wanafunzi wanakabiliwa na uhaba wa bweni.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa