Kamati ya Siasa Wilaya ya Iringa Yaridhishwa na Utekelezaji wa Miradi
Kamati ya Siasa Wilaya ya Iringa imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Januari 26, 2024. Hatua hii imefikia katika kuonesha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama Ilani inavyowahitaji kufanya hivyo.
Akitoa taarifa ya mradi katika Hospitali Teule ya Tosamaganga, Ndugu Agrey Mgeni Afisa Utumishi wa Hospitali hiyo amesema, “ hospitali hii ilianza kujengwa mwaka 1965 na kukamilika mwaka 1968 na vijana wa kundi la Manitese toka Torino Italia na Wamisionari wa Shirika la B.M. Consolata, na ilizinduliwa rasmi na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere Februari 17, 1970”.
Ndugu Mgeni ameendelea kusema kuwa, Hospitali imekua na kufikia hatua ya kutoa huduma za kibingwa, na bobezi na hivyo kusaidia wananchi wengi kupata huduma badala ya kwenda kutibiwa Mikoa mingine”. Amesema, kwa mwaka hospitali inahudumia wagonjwa katika 62,000 hadi 78,000 ikiwa ni wagonjwa 7,000 hadi 8000 ni akina mama wajawazito na watoto kwa kuwa huduma hizi ni karibu na bure”.
Aidha, Hospitali imeweza kununua mashine ya mionzi (CT Scan) kwa ajili ya kupima wagonjwa waliopata madhara kichwani. Hivyo kusaida wagonjwa wengi wanaokuja hapo wakiwa wamepata ajali mbalimbali.
Uongozi wa Hospitali hiyo wametoa ombi lao kwa Kamati hiyo kuwa, wanaomba wapewe laini ya umeme ya pekee kama hospitali ili kuokoa maisha ya wagonjwa hasa wanaohitaji oksijeni zinazoteemgea umeme. Na Kwamba wanaaomba mradi wa umeme ulioachwa na Serikali kwa miaka mingi ambao ulikuwa unazalisha KWV 60.
Pia wamewasilisha ombi la kujengewa Kituo cha Polisi kwani eneo hilo liko kando na Mji hivyo kuwepo na ulinzi wa kutosha. Kadhalika ombi la kusamehewa deni wanalodaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao ni zaidi ya kiasi cha Shilingi Milioni 200 zinadaiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Komredi Costantine Kihwele amesema, “nawapongeza kwa kutoa huduama nzuri hapa hospitali na kwamba mgonjwa hupona kwa kauli nzuri na kisha dawa zinamalizia. Naomba mashine hii itunzwe ili idumu muda mrefu”.
Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Ndugu Stanslaus Mhongole amekiri kuwa kuna chanzo ambacho kilikuwepo cha kuzalisha umeme, na kwamba ni suala la kukarabati tu miundombinu yake na tatizo hilo linaweza kuisha.
Ziara imeendelea hadi katika shule mpya ya Sekondari ya Weru iliyopo katika Kata ya Ulanda.
Shule hiyo ya Weru imeanza Kidato cha Kwanza Januari 08, 2024 na hadi sasa wanafunzi 128 wameripoti kati 148 waliopangwa shuleni hapo.
Kamati imeridhishwa na miradi hiyo na kupongeza uongozi wa Halmashauri ambao unaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Wakili Bashir Muhoja kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa