Chanjo ya nyongeza awamu ya pili yaendelea kutolewa katika Vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya. Chanjo hii ni muendelezo wa chanjo ya Polio (IPV2) ambayo inaambatana na chanjo ya kwanza ikiwa ni dozi ya kwanza.
Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya Mei 06, 2025. na kuhudhuriwa na viongozi wa Dini na Kisiasa.
Kulikuwa na chanjo ya kwanza ya matone na sasa ni chanjo ya sindano kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi miezi 9. chanjo hii husaidia kuzuia ugonjwa wa polio (kupooza), kifadulo na pepopunda hasa kwa watoto wadogo. Mtoto akikosa chanjo hii hupelekea ugonjwa wa kupooza na kuathiri hatua za ukuaji wa mtoto. Hivyo wananchi wote wanahimizwa kwenda kuwapatia chanjo hii watoto wao.
Akiongea katika uzinduzi wa chanjo hii awamu ya pili Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James amesema, “lengo la zoezi hili ni kuimarisha jamii yetu ili tuwe na uelewa wa pamoja. Viongozi wa Dini na viongozi wa Kisiasa ni jukumu letu sote kutoa ujumbe kwa wananchi wetu ili wajue umuhimu wa chanjo hii.
Mhe. Kheri ameendelea kusema, “Serikali imeona haja na hoja ya kulinda jamii yake dhidi ya magonjwa haya, na kutoa chanjo hizi ambazo zinatambulika kidunia. Wananchi wote wenye watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi miezi 9 wanasisitizwa kwenda kuwapatia chanjo watoto, kwani inatolewa bila malipo yoyote na kwenye vituo vyote vya kutolewa huduma za afya”.
Nao viongozi wa Dini na Siasa wamelipokea suala hili kwa umakini zaidi na wamekiri kwenda kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa zoezi hili.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa