Kampeni ya upandaji miti katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa mwaka 2024 imezinduliwa rasmi kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika shule ya sekondari Weru 27.01.2024. Zoezi hilo limeratibiwa na wadau wa mazingira kutoka shirika la EJESO kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti, Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndg. Johakim Mshana amesema, Halmashauri imezalisha miche ya kutosha kabisa kwenye vitalu vyake vilivyopo mnadani kata ya Izazi, Magubike kata Nzihi na kutoa wito kwa wananchi kufika kwenye maeneo hayo na kupewa miche ya miti bure”
Eidha TFS wana vitalu vyao katika kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa mahali ambapo wananchi wanaweza kufika na kupewa miche ya miti bure bila malipo yeyote kwa ajili ya upandaji.
“Kwa msimu huu wa mwaka 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inatarajia kupanda miti inayofikia Milioni tano na laki sita (5,600,000) katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri na ndiyo idadi ya miche ambayo imezalishwa tayari”, amesema ndugu Mshana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la EJESO ndugu Baton Madembwe amesema zoezi hili ni endelevu, litaendelea kwenye maeneo mbalimbali hadi June 05, 2024 kwenye kilele cha siku ya Mazingira duniani ambapo watakabidhi miti iliyopandwa tayari.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa