Kikao cha tathimini ya Mkataba wa Lishe Robo ya Nne kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilifanyika tarehe 22/08/2022 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo kikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Mohamed Moyo.
Katika kikao hicho Mwenyekiti ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja kwa kusimamizi wa ufanisi kwa utekelezaji wa viashiria vyote vya Mkataba wa Lishe Ngazi ya Wilaya ikiwemo utoaji wa fedha (toka mapato ya ndani) zilizopangea kwa ajili ya kutekeleza shughuli za lishe.
Aidha kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Halmashauri imeumia kiasi cha Tsh. 56,189,150/= sawa na asilimia 89.43% kwa watoto 46,677 ambayo ni Tsh. 1,203/= kwa kila mtoto chini ya miaka mitano katika fedha zilizopangwa.
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameongeza kusema kwa kusisitiza kuwa, wajumbe wote wakiwemo Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa viashiria vyote kufanya vizuri katika mwaka wa fedha unaoanza 2022/2023, ili kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja, amemshukuru Meshimiwa Mkuu wa wilaya kusimamia kwa karibu na kutoa msukumo katika utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa Lishe, na kuomba wajumbe wengine kufanya hivyo ili kuokoa jamii.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa