LEAD FOUNDATION YAKARIBISHWA IRINGA DC
Lead Foundation ambalo ni Shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza miradi ya uongozi, uhifadhi wa mazingira, pamoja na maendeleo ya Jamii limekaribishwa kufanya shughuli zake Iringa hususani katika katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo vijiji vilivyoteuliwa kwa kuanzia ni Malizanga, Magombwe na Isele.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadau mbalimbali wa shirika la Lead Foundation yaliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo – Iringa Novemba 01, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amesema, “Ujio wa Lead Foundation pamoja na program zake ni ujio ambao tunaupokea kwa mikono miwili, tunawakaribisha Lead Foundation kwa sababu tunaamini wanaenda kuongeza juhudi za Halmashauri katika utunzaji wa mazingira, wanakwenda kuunga mkono jitihada za serikali yetu katika usimamizi wa sera ya mazingira”.
Aidha Mhe. Kheri ameahidi ushirikiano kwa niaba ya serikali ili kuhakikisha lengo husika la shirika linafikiwa na kwamba ni matazamio yake kwamba Wilaya ya Iringa inaenda kuwa Wilaya ya mfano katika namna bora ya kurejesha uoto wa asili uliopotea kwa baadhi ya maeneo.
Naye Mkurugenzi wa Programu ya Lead Foundation Ndg. Njamas Chiwanga amefafanua kuhusu njia ambazo shirika linatumia ili kufikia lengo lake la uhifadhi wa mazingira ambacho ndio kipaombele katika utekelezaji wa shughuli za shirika na shughuli zingine za maendeleo ya jamii au motisha kwa jamii zinazozunguka eneo la mradi.
Lead foundation inashirikiana na wadau wengine ikiwa ni pamoja na Nawiri Foundation, sanjari na taasisi mbalimbali za serikali na jamii kwa ujumla katika kutekeleza miradi yake.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa