Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa Ndug. Michael Semindu Leo June 15,2024 ameongoza Wafanyakazi wa Halmashauri kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyo fanyika katika Kata ya Lumuli Kijiji cha Muwimbi
Katika Hotuba yake Semindu amesema lazima tukubaliane kama Jamii kwamba, kukuza maarifa ya Watoto, Serikali imeweka Sera nzuri ya kukuza maarifa kama vile Uboreshaji Mitaala ya Kufundisha, TEHAMA yaani Sayansi na Teknolojia , mafunzo katika Vyuo vya Juu na Kati pamoja na utoaji elimu kwa ujumla wake.
Kwa upande mwingine Ndugu Semindu amesisitiza kuwa Serikali imeshirikisha viongozi wa Mila, Dini, kuchaguliwa na kuteuliwa, wajasiriamali ili kuweza kufikisha elimu hii kwa watoto na kusisitiza kutatuliwa kwa changamoto kama vile matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari, mmomonyoko wa maadili kwa jamii yetu, Wazazi au Walezi kutotimiza wajibu wao pamoja na Mila na Desturi zilizopitwa na wakati kama vile kukandamiza watoto wa jinsia moja kuwa wana haki kuliko wengine.
Pamoja na hayo Bwn. Semindu amesema Serikali imekabiliana na changamoto hizo kwa kuhakikisha elimu ya malezi na makuzi ikitolewa kwa wazazi hususani na lishe bora kwa mtoto. Mtoto ni lazima alindwe dhidi ya vitendo vya ukatili kam kupigwa, kuchomwa moto na wazazi kuimarisha mahusiano na mawasiliano na watoto tunaowalea ili kuwa rahisi kujua mtoto ana changamoto ipi.
Vilevile Ndugu Semindu amewaomba Watalamu wa Maendeleo ya Jamii kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na haki sawa. Maana jamii imekuwa ikiamini kuwa ni lazima kuwe na jinsia mbili tofauti kwenye nafasi yeyote huku Kuna wengine wakipoteza nafasi. Kwa mfano nafasi ziko tano na wanawake wote ndo wanasifa wapewe wote ili kutimiza haki sawa kwa kila mtu.
Pamoja na hayo Ndugu Semindu ametoa shukrani kwa Wadau waliowezesha shughuli hiyo kufanyika kama vile Word Vison, Asas group, Compassion, Tahea na Care.
Kauli Mbiu katika Maadhimisho haya inasema, "Elimu Jumuisho kwa Watoto Izingatie, Maarifa, Maadili na Stadi za Kazi".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa