Maandalizi ya Miradi ya Boost
Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya kujenga miundombinu mbalimbali. Katika utekelezaji wa miradi hiyo, Program ya Boost nayo inaendelea kutekelezwa kwa awamu nyingine.
Kata ya Mlenge ni miongoni mwa Kata 28 za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo imebahatika kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya katika Kijiji cha Kinyika. Kiasi cha Shilingi Milioni 350 kimepokelewa kwa ujenzi huo ambao kutakuwa na madarasa 9, jengo la Utawala, vyoo vya wanafunzi na Walimu na madarasa 3 ya elimu ya awali na vyoo vyao.
Aidha, katika Kata ya Ilolompya kutakuwa na ujenzi wa madarasa 2 ya elimu ya awali, uzio na vyoo.
Hii ni agizo la Serikali kuwa, kila mwaka kuwepo na miundombinu mizuri ya kuwafanya watoto wapende shule.
Timu ya Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji/Kata husika Julai 18, 2024 imeweza kukagua maeoneo ambayo itajengwa shule hiyo mpya na madarasa ya elimu ya awali kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Wananchi wamepokea miradi hiyo kwa mikono miwili na wapo tayari kutoa ushirikiano nguvu kazi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa