“Mabilioni Haya ya Fedha za Miradi, Yatumike Kama Ilivyokusudiwa”, Mwenyekiti Mhapa
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 umekamilika leo Mei 25, 2023 ambapo ulianza jana Mei 24, 2023 kwa kutoa taarifa za Kata.
Akitoa hotuba yake fupi katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Stephen Mhapa amesema, “Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuletea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali. Fedha hizo zimelenga katika Sekta ya Elimu, kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu ili watoto wetu waweze kusoma kwa utulivu, hivyo zitumike kama lengo lilivyokusudiwa, na kwamba ujenzi ufuate sheria za manunuzi”.
Mheshimiwa Mhapa ameongeza kusema kuwa, “nawaomba Waheshimiwa Madiwani kusimamia vema ujenzi huo kwa kushirikiana na Wataalamu, ili kazi hii iwe nyepesi na ikamilike kwa wakati”.
Fedha Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya miradi ya BOOST kwa shule za Msingi, Shilingi Milioni 347 kwa ujenzi wa mabweni 2 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Ifunda, Shilingi Milioni 576 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni 3, Madarasa 6 na vyoo matundu 18 kwa Shule ya Sekondari Idodi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy ametoa neno katika Baraza hilo kwa kusema, “Nawapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa kusimamia vema miradi ya maendeleo. Pia nawaomba kuendelea kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yetu sambamba utunzaji wa vyanzo vya maji,kwani suala hili ni la Kitaifa zaidi. Imetengwa siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya kufanya usafi kila mahali, hivyo yatupasa kusimamia na bila kusukumwa”.
Mheshimiwa Kessy pia amesisitiza suala la ukusanyaji wa mapato, kwani ndiyo msingi wa kila Halmashauri. Pia katika
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Komredi Costantine Kihwele amesema, “mimi kama Mwenyekiti wa Chama naridhishwa na utendaji kazi wa Madiwani pamoja na Wabunge wa majimbo yote mawili ya Kalenga na Isimani. Pamoja na ugeni tunaotegemea kupokea ambao ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comredi Daniel Chongolo, tunatakiwa kumpokea kwa shangwe na tuwe naye kwenye ziara yake yote katika Halmashari, na kuwasisitiza wananchi kuwepo kwenye maeneo ambayo atapita kukagua miradi”.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Mathew Nganyagwa naye ametoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa kusimamia miradi, na kutoa uchambuzi wa miradi hiyo kwa uwazi. Pia ametoa pongezi kwa Wabunge kwa kujitoa kufuatilia fedha na kushawishi ili kuleta miradi katika Halmashauri. Aidha amewashukuru Wadau mbalimbali kwa kufanya kazi katika Halmashauri na kumuomba Mkurugenzi kuwa, Awashukuru Wadau hao kwa vitenda kwa kuwapa tuzo na vyeti
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa