Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka mafundi kuongeza kasi kwenye miradi ya ujenzi waliyopewa kuitekeleza katika maeneo mbalimbali. Ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea nakukagua utekelezaji wa miradi kwa siku ya pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa April 24, 2024.
Katika miradi aliyoitembelea na kuikagua Mhe. Serukamba amejiridhisha kuwa kwa sehemu kubwa vifaa sio changamoto bali ni mafundi kuongezeka katika kila mradi ili kuongeza kasi katika utekelezaji wake
Aidha Mhe. Serukamba ametoa tahadhari kwa mafundi watakaosua sua kwenye kazi walizopewa kwamba huenda wasipewe kazi tena, hivyo mafundi wote wanapaswa kukamilisha kazi kwa wakati kwa kadri ya makubaliano.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa kwa siku ya pili ni ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Kiwere, ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na matundu 8 ya vyoo katika shule ya sekondari Kiwere, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Itagutwa, ujenzi wa matundu 6 ya vyoo shule ya sekondari Ilambilole, ujenzi w vyumba 3 vya madarasa shule ya sekondari Isimani na ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na matundu 4 ya vyoo katika shule ya sekondari Furahia.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa