Magiri Azipongeza Halmashauri Kufanikiwa Kampeni ya Usafi na Mazingira
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Peresi Magiri amewapongeza viongozi wa Halmashauri, wadau na wananchi wote kwa kuweza kutekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi na mazingira.
Kwa kuhakikisha wanafanya usafi na pia kuhakikisha kaya zote zina vyoo bora lengo ni kujikinga na magonjwa yatokanayo na uchafu kama vile kipindupindu, kuhara, na magonjwa mengine ya mlipuko.
Ameyasema hayo katika Maadhimisho ya wiki ya usafi na siku ya choo duniani ambapo Mhe. Magiri amekua Mgeni Rasmi katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Kimkoa katika viwanja vya kichangani vinavyopatikana katika Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa huku yakibeba kaulimbiu isemayo “kuyafanya yasiyoonekana kuonekana”
Sambamba na hilo pia Mhe. Magiri amekabidhi vyeti pamoja na vikombe kwa Halmashauri nne zilizofanya vizuri ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kampeni ya usafi na mazingira ambapo vyeti hivyo pamoja na vikombe vilipokelewa na wawakilishi wa maeneo husika na amewaomba kuendeleza kutunza mazingira kwani kwa kufanya hivyo wataweza kulinda afya za wananchi.
Pia Maadhimisho hayo yameambatana na maonesho mbalimbali yenye lengo la kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na usafi wa binadamu, watengenezaji wa dawa za asili zitokanazo na mimea, bustani, watengenezaji wa malighafi zitokanazo na plastiki, pamoja na njia za utunzaji wa mazingira kupitia usafi wa vyoo.
Aidha taarifa mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo taarifa ya mganga mkuu wa mkoa iliyotolewa na kaimu mganga mkuu wa mkoa Dkt. Credianus Mgimba ambapo amepongeza jitihada mbalimbali zinazoendelea kutolewa na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingaira na kusema kwamba kama Mkoa unaelekea pazuri nakuomba Halmashauri zote kuendeleza jitihada hizo.
Pamoja na yote pia wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo wakiwemo watendaji wameonesha kufurahia maadhimisho hayo huku wakipongeza waandaaji wa vyeti na vikombe kwani inawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kutunza na kuyalinda mazingira.
Ikumbukwe kuwa maadhimisho hayo yalianza tarehe 13/11/2022 na kufikia tamati tarehe 19/11/2022 ambapo kitaifa yatafanyika katika Mkoa wa Dodoma yakiwa na ujumbe usemao [KUYAFANYA YASIYOONEKANA KUONEKANA].
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa