Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, Zahitimishwa Mkoani Iringa
Hatimaye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zahitimishwa kukimbizwa Mkoani Iringa na kukabidhi Mkoani Morogoro. Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mkoani Iringa Mei Mosi 2023 na kukimbizwa kilometa 719 na miradi 31 yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 63.1.
Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa Mkoani Morogoro na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 6, 2023 na Mh. Fatuma Mwasa, katika Wilaya ya Mlimba Kata ya Chita ukiwa salama na wakimbiza Mwenge Kitaifa 6, Wakufunzi 2, na Maafisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais 3 wakiwa na afya njema.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023 inasema,
“Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji, Kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa