MBOMIPA Wakabidhiwa Gari kwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyama Pori
MBOMIPA ni Jumiya ya Uhifadhi ya Wanyama Pori katika vijiji 21 vilivyo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Jumuiya hii husaidia ulinzi wa majangiri katika kulinda Hifadhi na kwamba wamejiwekea taratibu mbalimbali ili kudumisha hifadhi.
Katika kushirikiana na Taasisi nyingine kama Kilombelo North Safari’s, Taasisi hiyo iliahidi kununua gari ambayo itawasidia MBOMIPA katika kufanya doria mbalimbali hifadhini.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Aprili, 2025.
Taasisi hiyo ya Kilombelo North Safari imetimiza ahadi yake kwa kununua gari aina Toyota Hilax na kuikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, ili aweze kuikabidhi kwa Jumuiya ya MBOMIPA kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.
Akiongea katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano Ndugu Dotto Wilson Sadala Afisa Mahusiano na Jamii wa Kilombelo North Safari’s amesema, “gari hii imenunuliwa kiasi cha Dola 30,000 sawa na fedha ya Tanzania kiasi cha Milioni 70, leo tunaikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ili awakabidhi Jumuiya ya MBOMIPA”
Akipokea gari hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Heri James amesema, “Gari hii itatusaidia katika shughuli za ufuatiliaji na ulinzi kwenye hifadhi yetu, hivyo naomba wananchi tuwe marafiki wa mazingira na uhifadhi”. Pia tujue namna ya kuishi na wanyama, kwani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina fursa nyingi, tunawakaribisha Wawekezaji wengi kuja kuwekeza”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa