Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amefanya kampeni katika Jimbo la Ismani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kumnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge wa jimbo la Isimani, William Lukuvi, na wagombea wa nafasi za Udiwani katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Itunundu, tarafa ya Pawaga mkoani Iringa Septemba 25, 2025.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi, Dkt. Nchimbi amesema iwapo CCM kitapewa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi, serikali itazidi kuboresha miundombinu ya barabara, kukuza kilimo cha umwagiliaji na kuimarisha sekta ya mifugo ili kuongeza tija kwa wananchi.
Aidha, amewataka wananchi wa Isimani kuendelea kuiamini CCM na kuwachagua wagombea wake katika nafasi zote za udiwani, ubunge na urais, akisisitiza kuwa chama hicho kina historia na uzoefu mkubwa wa kutekeleza miradi ya maendeleo inayoendana na mahitaji ya wananchi.
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa CCM jimbo la Isimani, William Lukuvi, ameahidi kuendeleza jitihada za kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo, hususan katika kuboresha huduma za kijamii na kuinua hali ya uchumi wa wakulima na wafugaji.
Uchaguzi Mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025
#kurayakohakiyakojitokezekupigakura
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa