Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassain afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,awataka wakafanye kazi.
Ummi Mohamed(Afisa Habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.Samia Suluhu Hassain leo amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri leo Machi 31 mwaka 2021, baada ya Mh.Dkt. Philip Mpango kula kiapo cha kuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano liliwasilishwa Machi 30 mwaka huu na kuthibitishwa na Bunge kwa asilimia mia moja,sanjari na tukio hilo Mh.Rais amemteua Mh.Balozi Hussein Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Mh.Rais pia,amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifutavyo; Mh. Dkt.Mwigulu Nchemba amekwenda Wizara ya Fedha na Mipango akitokea Wizara ya Katiba na Sheria,Mh.Paramagamba Kabudi amerudi Wizara ya Katiba na Sheria, Mh.Ummy Mwalimu ameenda Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akitokea Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambapo nafasi hiyo imechukuliwa na Mh.Suleiman Jafo ambaye ametoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Aliyekuwa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mh.Huruma Mkuchika amepangiwa kazi maalum na nafasi hiyom ikichukuliwa na Mh.Mohamed Mchengelwa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Libelata Mulamula,Wizara ya Viwanda na Biashara Mh.Kitila Mkumbo,Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mh.Geophrey Mwambe.
Mh.Rais pia,amefanya mabadiliko hayo na kwa Manaibu Waziri kama ifutavyo;Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Pauline Gekul,Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh.Mwanaidi Ally Hamisi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Mbarouk Mbarouk, Wizara ya Katiba na Sheria,Mh.Geophrey Pinda, Ofisi ya Makamu wa Muungano na Mazingira Mh.Hamad Said Chande, Wizara ya Fedha na Mipango Mh.Masauni Hamad Masauni, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mh William Ole Tate.
Pia,amewateuwa wabunge ambao baadhi yao wamepangiwa majukumu katika Wizara mbalimbali ambao ni Mbarouk Mbarouk na Libelata Mulamula, na Dkt.Bashiru Ally Kakurwa ameteuliwa kuwa Mbunge.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa