AMREF yatambulisha Mradi mpya wa Maji na Maendeleo – (Water And Development Alliance)
Zaituni Omar (Iringa-DC)
Mhandisi wa Mradi wa Maji na Maendeleo -WADA, Dickson Watson ametambulisha Mradi huo jana tarehe 3 mwezi Februari mwaka huu katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilioyopo katika Kijiji cha Kalenga Mradi ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 12.
Akielezea gharama za Mradi Mhandisi Watson amesema jumla ya fedha za kimarekani dola 669,565 ambazo sawa na fedha za Kitanzania shilingi Milioni 160,126,470, zitahudumia katika Vijiji 5 ambavyo ni; Kijiji cha Nyabula, Mlanda, Ndiwili, Mkungugu, na Nyango’oro.
Aidha Mhandisi huyo alisema kwa kuwa Mradi huu unatekelezwa katika Mkoa mzima wa Iringa tayari Tarehe 28 mwezi Januari Mradi huo ulizinduliwa Kimkoa na katika Wilaya ya Ieringa ni ni Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndio itanufaika na mradi huo katika Vijiji vitano ambavyo nimevitaja hapo awali.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Ponsiano Kayage akitoa shukrani kwa Shirika hilo la AMREF, kwa kuchagua kufanya Mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuwa ina Vijiji vingi, lakini pia Shirika hilo litakuwa linaunga mkono jitiohada za Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo.
“Kwa niaba ya Halmashuri nimefurahi AMREF kutuamini na kutupa Vijiji vingi katika Mradi huu kwani Kimkoa ni sisi ndio tumepata vijiji vingi na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa hatua zote za utekelezaji wa Mradi huu”alisema Mh.Kayage na kuongeza kuwa;
“Katika kuhakikisha Mradi huo unakwisha kwa ubora unaokusudiwa,sisi Viongozi tutakuwa tukisimamia suala zima la uwazi na uwajibikaji” alisema.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja kwa upande wake ameshukuru kwa kupata mradi huo, ambao anaamini utapunguza kero kwa kiasi kikubwa katika shule na vituo vya afya vilivyokuswa na mradi huo.
“Kwanza nishukuru,lakini pia niwapongeze AMREF kwa andiko lililopelekea kupata fedha ambazo leo hii na sisi wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Iringa tumekuwa wanufaika wa mradi”alisema Wakili Muhoja.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa