“Natoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Isimani, Mwenyekiti wa Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani wote, Mkurugenzi na timu yake ya Wataalamu kwa kufanikisha miradi hii iliyomalizika na inayoendelea katika Halmashauri hii. Kweli nimefarijika sana kuona miradi inapendeza na ipo katika hali nzuri”. Haya yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Innocent Bashungwa, wakati wa ziara yake kukagua miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Mheshimiwa Bashungwa amefanya ziara hiyo ya siku moja tarehe 04/07/2022 na kutembelea miradi mbalimbali katika maeneo ya Kituo cha Afya Kising’a, Shule ya Sekondari Isimani, Kituo cha Afya Isimani, shule ya Sekondari Nyang’oro, Shule ya Sekondari Izazi, na kituo kipya cha Afya cha Migoli ambacho kinaendelea na ujenzi.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Bashungwa ametoa maelekezo kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuwa, kutumia kiasi cha mapato ya ndani kumalizia miradi ambayo imesimama, ambapo ni baadhi ya maabara za shule na vituo vya afya, jengo la upasuaji, jengo la Utawala Isimani sekondari vikao vya Bodi kuelekeza elimu bila malipo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Isimani Mheshimiwa William Lukuvi, amemshukuru Mh. Bashungwa kwa kuja kutembelea Jimboni kwake na kukagua baadhi ya miradi ambayo ipo katika utekelezaji, na kumuomba tena fedha kwa ajili ya kufanya umaliziaji katika miradi iliyokwama kama maji, majengo ya madarasa, maabara na maktaba za baadhi ya shule, mabwalo na nyumba za watumishi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Queen Sendinga, ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Bashungwa kwa ujio wake na kwamba ametamani kuendelea kufanya ziara katika Mkoa wa Iringa ili ajionee mengi yanayofanyika mkoani humo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa