Mhe. Kayugwa Achaguliwa Kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa
Kama ilivyo ada kila mwisho wa mwaka wa fedha kunakuwa na uchaguzi wa kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani. Hivyo Baraza limeketi Oktoba 04, 2024 na kufanya uchaguzi hatimaye Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo amepatikana ambaye ni Mhe. Benitho Kayugwa.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa Mhe. Kayugwa amesema, anashukuru kwa kuaminiwa na kumpa kura nyingi ili aweze kuwa msaidizi wa Mwenyeiti wa Baraza la Halmashauri. Ameahidi kutoa ushirikiano na atafanya kazi kwa nguvu zote ili kufikia malengo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Stephen Mhapa amempongeza Mhe. Kayugwa kwa kuchaguliwa kwake, na kwamba ana uhakika na utendaji wake wa kazi, na kwamba Wahe. Madiwani wampe ushirikiano.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa