Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Kheri James amezindua Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi katika hafla iliyofanyika katika ukumbu wa Lutheran Iringa Novemba 01, 2024
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhe. Kheri amesema Jukwaa hili ni kiunganishi kikubwa sana kati ya wanawake na taasisi za kifedha na taasisi zingine za kiuchumi ambazo zinawaunganisha wanawake wote na fursa zilizopo.
“Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tayari imewatengea zaidi ya Shilingi Milioni 600 ambazo zinasubiri kukopeshwa wanawake wa Wilaya yetu ya Iringa, fedha hizi ni kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na wenzetu wenye mahitaji maalumu. Amesema Mhe. Kheri.
Aidha Mhe. Kheri amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utatuzi wa baadhi ya changamoto ikiwemo changamoto ya upatikanaji safi na salama ambapo kwa Iringa upatikanaji wake upo kwa Zaidi ya asilimia 80, huduma ya afya imeboreshwa sanjari masuala ya mitaji.
Vilevile Mhe. Kheri ametoa wito kwa wanawake kusaidia kwenye changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo suala la malezi ya watoto kwani malezi bora ya watoto ndio msingi na mtaji bora kwenye familia, na hili dio jukumu mama la mwanamke nyumbani.
Pia suala la udumavu limepewa msisitizo kwamba njia bora ya kuondokana na udumavu ni kula chakula bora ambacho kinaweza kisiwe cha gharama kubwa na kipo kwenye mazingira yetu na hata kwa upande wa shuleni watoto wanapaswa kula chakula ili wasome vizuri.
Naye mwenyekiti wa Jukwaa hilo Mhe. Ritha Mlagala ametoa pongezi kwa wadau wote wajukwaa na kuahidi kuwa yote yaliyotolewa wanayachukua kwa ajili ya utekelezaji
Jukwaa la uwezeshaji wananchi kiuchumi limeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kujenga na kumiliki uchumi wa nchi yao, kuwapatia watanzania fursa katika shughuli za uchumi, kuhamasisha na kuhimiza wananchi juu ya umuhimu wa uwekaji wa akiba, uwekezaji na ushirikishwaji kwa wananchi kwenye shughuli za kujiongezea kipato,kuwahudumia wananchi bila upendeleo pale wanapohitaji kuwawezesha kupitia huduma zinazotolewa katika wa kila siku.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa