Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa ufafanuzi juu ya wanaopaswa kufanya kazi kwenye miradi ya TASAF ya kwamba wazee watoto na watu wenye changamoto za kiafya hawapaswi kwenda kufanya kazi kwenye miradi ya TASAF inayoibuliwa kwenye maeneo mbalimbali nchini bali wenye nguvu hasa kwenye kundi la vijana ndio wanaopaswa kujitolea na kuwasaidia wazee.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na wanufaika wa mpango wa TASAF pamoja nawananchi wa kijiji cha Nyang’oro, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tar 23.11.2023 baada ya kukagua miradi inayotekelezwa na wanufaika wa mpango wa TASAF ambayo ni uchongaji wa barabara na ujenzi wa daraja.
“Maelekezo yapo wazi, kundi la watoto na wazee hawaruhusiwi kufanya kazi lakini maelekezo ya TASAF yanatoa nafasi kwa wanakaya walio na nguvu kujitolea kwenda kufanya kazi kwaajili ya kuwasaidia wazee,” amesema Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Eidha Mhe. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma zake za kuweza kutoa fedha kwaajili ya kusaidia kaya masikini waweze kujikimu kwenye mahitaji yao, na kuwaasa wanaopata feha za mpango wa TASAF wazitumie kwa kutimiza masharti yaliyowekwa ikiwemo kuwapeleka watoto shule na kuwatimizia mahitaji ya kiafya kama kuwapeleka kliniki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Wakili Bashir Muhoja ametoa pongezi zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya uwezeshaji wa kifedha kwa miradi mingi inayotekelezwa na iliyotekelezwa karibia kila kijiji ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, miradi ya maji, miundombinu ya barabara nk.
Katika kijiji cha Nyang’oro kaya 179 zimetambuliwa na kuandikishwa ambapo kijiji kimepokea jumla ya Tsh. 33,350,000 kwa awamu 7 ikiwa ni ruzuku zawalengwa na uendeshaji wa miradi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa