Mhe. Ulega Afanya Ziara Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maendelo
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Oktoba 02, 2024. Lengo la ziara yake ni kukagua miradi ya maendeleo na kuzindua kwa miradi ambayo imekamilika.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Ulega amesema, kwanza anamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuja kukagua miradi ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, na kujionea maendeleo yanyofanywa na Halmashauri hiyo.
Mhe. Ulega ametoa rai kwa uongozi wa Mkoa na Wilaya na Halmashauri kusimamia miradi ambayo bado haijakamilika, iongezwe kasi ili ikikamililika ianze kutumika kwa wakati.
Aidha katika ziara yake amepata nafasi ya kuongea na wananchi na wanafunzi waliopo kwenye maeneo aliyopita na kuwasisitiza kusoma kwa bidii ili waje kuwa viongozi wazuri baadae na kuwa na tabia njema.
Upande wa wananchi wamesisitizwa kutunza miradi inayoletwa na Serikali kwani miradi hiyo ipo kwa ajili ya wananchi wenyewe. Pia kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kila jambo, kwani wananchi wana deni kubwa kwa Mhe. Rais kutokana na fedha nyingi alizotoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbalipa kumuombea dua Rais wetu.
Mhe. Ulega ameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi kwa kutoa jezi na mipira kwa shule za Ifunda, Kiwele, Pawaga na Mboliboli, pia kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa Kata hizo nne.
Katika ziara hiyo, wananchi wamepongeza kwa ujio wake na kumuahidi Mhe. Rais kulipa deni hilo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 pia katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025,
Baadhi ya miradi aliyoteembelea Mhe. Ulega ni kuzindua jengo la bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, Kuzindua majengo ya madarasa katika Shule ya Sekondari Kiwele, kuzindua majengo ya madarasa na bweni katika Shule ya Sekondari Pawaga, na kuzindua majengo ya madarasa katika Shule ya Sekondari Mboliboli.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa