Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekula kiapo akiwa na Manjozi tele.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa-DC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.samia Suluhu Hassan amerudia kuwajulisha Watanzania wote juu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena iliyopo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya tatizo la mfumo wa umeme kwenye moyo ambalo alikuwa nalo kwa Zaidi ya miaka kumi.
Mh.Rais amesema nchi yetu itakuwa katika maombelezo kwa siku 21 na siku mbili kati ya hizo tarehe 22 na tarehe 26 zitakuwa siku za mapumziko kwakuwa siku ya tarehe 22 mwili wa aliyekuwa Rais Dkt.Magufuli utaagwa Dodoma na siku ya tarehe 26 aliyekuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli atapumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Aidha vitabu vya maombolezo kwa kila mtu atakayependa kusaini vinapatikana maeneo yafutayo; kwa Dar es Salaam vitabu vitakuwa Ukumbi wa Karimjee na Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dodoma viwanja vya Nyerere Square,Chato ofisi ya Mkuu wa Wilaya Zanzibar jingo la zamani la Baraza la Wawakilishi na Ofisi zote za Wakuu wa mikoa na Wilaya.
Pia,vitabu vitapatikana Ofisi zote za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania nzima na Ofisi zote za Balozi za Tanzania nje.
“Ndugu Watanzania leo sio siku nzuri kwangu ya kuhutubia maana nimeelemewa na kidonda na mzigommkubwa moyoni mwangu,kiapo nilichokula leo ni tofauti na viapo vyangu vyote vya awali nilivyoapa kwa faraja,nderemo na vifijona bashasha tele leo nimekula kiapo cha juu kabisa katika nchi yetu ya Tanzania nikiwa na majonzi tele hivyo mtaniwia radhi nitaongea kwa uchache na ufupi sana nitatafuta wasaa mwingine hapo baadae tuzungumze na kukumbushane na kuwekana sawa”alisema Mh.Rais Samia Suluhu Hassan.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa