Miradi 8 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 6.6 Yakubalika na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023
Mwenge wa Uhuru Wakimbizwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 04/05/2023, kwa Kilometa 91.02 na kufanikiwa kupitia miradi 8 yenye jumla ya Shilingi za Kitanzania Bilioni Sita Milioni Mia Sita Ishirini na Sita, Laki Tano na Ishirini na Sita Elfu Mia Saba Orobaini na Nane na Senti Sabini na Tatu (Tsh. 6,626,526,748.73), ambapo umekagua miradi 3, umezindua miradi 2 na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi 3 pamoja na kuzindua Klabu ya Kuzia na Kupambana Rushwa, Klabu ya Mapambano ya Dawa za Kulevya na Klabu ya Mazingira.
Mwenge ulipokelewa Kijiji cha Negabihi kilichopo Kata ya Magulilwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Mwenge umefanya mbio zake katika Jimbo la Kalenga, Tarafa za Mlolo na Kiponzero kwenye Kata za Magulilwa, Lyamgungwe Mseke, Mgama, Ifunda, kwa vijiji vya Negabihi, Magulilwa, Kikombwe, Ugwachanya, Wenda, Mlandege, Ihemi na Ifunda, ambapo mkesha ulifanyika katika Kijiji cha Ifunda na hatimaye kwenda kukabidhi Halmashauri ya Mji Mafinga tarehe 05/05/2023.
Mwenge umeridhia miradi yote 8 iliyopitiwa kwa kukagua nyaraka mbalimbali za hatua mbalimbali za miradi.
Kauli Mbiu ya Mwenye wa Uhuru kwa Mwaka 2023 ni “Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji, Kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa