Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja ameongoza watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye zoezi la upandaji miti katika eneo la makao makuu ya Halmashauri yaliyopo kijiji cha Ihemi Februari 21,2024.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri wakati wa zoezi la upandaji miti, Wakili Muhoja amesema kuwa hili ni zoezi la kitaifa hivyo kila mtumishi anapaswa kushiriki kupanda miti na kuitunza iweze kukua na itakuwa kumbukumbu nzuri sana kwa baadaye.
Eidha, kwenye suala la maji kwa ajili ya umwagiliaji Wakili Muhoja amewahakikishia watumishi kuwa ameshaongea na Mhandisi wa Ujenzi kwa ajili ya kuona namna ya kuvuna maji ya mvua kupitia gata zilizopo kwenye majengo ya Halmashauri sanjari na kuwashirikisha wadau wa maji kutoka RUWASA ili kuwa na uhakika Zaidi kuhusu suala la maji.
Katika zoezi hili, miti Zaidi ya mia mbili imepandwa kuzunguka majengo ya Halmashauri ambapo kuna miti ya matunda ya aina mbalimbali na miti ya vivuli. Zoezi la upandaji miti linaendelea katika maeneo mbalimbali ya halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo Halmashauri inashirikiana na wadau wake mbalimbali kama One Acre Fund, na wakala wa Misitu (TFS) kuhakikisha kuwa miti ya kupanda inapatikana sambamba na uhamasishaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa