Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndg. Robert Masunya amepokea vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi vyenye thamani ya Tsh. 1,635,000/-ambapo vifaa vingine vyenye thamani kama hiyo vinatarajiwa kwenda Shule ya msingi Kipera inayohudumia watoto wenye mahitaji maalumu kutoka shirika la IBO.
Mapokezi ya vifaa hivi yamefanyika katika ukumbi mdogo wa Siasa ni Kilimo Iringa Mei 27, 2024. Vifaa vilivyopokelewa ni mipira ya miguu(football), mipira ya mikono (hand ball), mipira ya wavu (volley ball), Mipira ya pete (netball), mikuki na jezi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ndugu Masunya amesema, Iringa DC inatambua na kuthamini mchango wa IBO kwenye Halmashauri na kwamba vifaa vilivyopokelewa vitatumika kama ilivyokusudiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa shirika la IBO pale kunapokuwa na uhitaji.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji ndugu Masunya amepata fursa ya kuongea na Wakuu wa shule za Sekondari akiwasisitiza juu ya uadilifu, ubunifu na uzalendo katika usimamizi wa miradi iliyopo kwenye maeneo yao. Ndugu Masunya ameongeza kuwa ni muhimu sana kwa wakuu wa shule kuwajengea uwezo watu waliochini yao ili kuleta ufanisi katika utendaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa