Mhe. Sendiga Ahimiza Ushirikiano Upatikanaji wa Hati Safi H/W Iringa
Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa umefanyika leo tarehe 10/06/2022 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo, na kuhudhuriwa na Viongozi wa Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Quen Sendiga, Katibu Tawala Mkoa Bibi Happiness Seneda pamoja na wataalam wengine kutoka ngazi ya Mkoa.
Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kujadili taarifa ya majibu ya hoja za Mkaguzi wa nje kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia 30, 2021, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amesema.
Katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiwa mi moja ya Taasisi ya serikali, ilifunga hesabu zake na kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa ajili ya ukaguzi. Katika Mwaka huo wa ukaguzi Halmashauri ilipata hati inayoridhisha.
Lakini pia amesema katika ukaguzi huo, jumla ya hoja 31 zilizotolewa na kujibiwa, kati ya hizo sita (6) zimehakikiwa na kufungwa, hoja 14 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaj, hoja 10 utekelezaji wake haujakamilika, na hoja 1 imerudiwa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa MHe. Stephen Mhapa amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuendele akuzifanyia kazi hoja zote ambazo zimeibuka kwa wakati pamoja na kuchukua hatua stahiki.
Naye Katibu Tawala Mkoa Bi Happines Senedsa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata hati safi kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022, na kusema hoja zote ambazo zimeibuka zifanyiwe kazi, kadhalika ametoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuwachukulia hatua watumishi ambao ni wabadhilifu.
“Tuna watumishi watatu ambao tayari tumeshawachukulia hatua lakini pia niwatake viongozi wa Halmashauri kuendele kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati, hasa ule wa Makao Makuu ya Halmashauri, na Vituo vya Afya”.
Naomba kusisistiza pia kuhusu umoja, Umoja pia ni jambo la msingi na muhimu, kwani umoja utasaidi kufikia malengo ambayo tumejiwekea kama Halmashauri lakini pia itasaidia kuheshimiana katika kazi. Ameongeza.
Akitoa hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga naye ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 japo amesema nguvu iliyotumika ni kubwa mno.
Amesema kuwa ni vyema kama viongozi kuwepo na ushirikiano wa pamoja lakini pia ameutaka ushirikiano huo kuiweza kusaidia kutumika katika kutatua hoja zote zilizopatikana.
“Hadi sasa kuna hoja 58, 18 zinafanyiwa kazi, 24 za 2020/2021 na 17 ni za miaka ya nyuma, 10 zimeshughulikiwa na kubaki na hoja 41. Hivyo hoja 17 za nyuma lazima zifanyiwe kazi kwa wahusika kuwachukulia hatua. Amesema.
Sambamba na pongezi pia Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Seniga ametoa maagizo na maelekezo kwa Halmashuari ya Wilaya ya Iringa ikiwemo kujua kwa mapana viashiria vinavyosababisha hoja, kufuata utaratibu kwenye manunuzi ya Halmashauri pamoja na kufuatilia kesi zote zilizopo mahakamani.
“Tufuate ushauri wa wakaguzi wa ndani na nje ili kupungunguza hoja, pale taarifa za Mkaguzi wa ndani inapotolewa basi Halmashauri iweke utaratibu mzuri wa jinsi ya kudhibiti hoja hizo. Amesema.
“Niwatake muweze kufuatilia kwa ukaribu mashine za ukusanyaji wa mapato (POS) zote zinazokusanya fedha, kuwa zinafanya kazi muda wote, pia kuna baadhi ya mashine hazijafanya kazi kwa takribani siku 400 nazo zifuatiliwe”.
Kadhalika ameongeza kwa kusema makato ya watumishi yapelekwe kwenye mifuko husika, na kuhusu zoezi la Sensa ni zoezi la kitaifa hivyo amesisitiza kujitokeza na kuhamasisha wengine ili kusaidia ukamilikaji wa zoezi hilo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa