Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema kuwa hakuna kilele wala kufunga maadhimisho ya kupinga Ukatili wa kijinsia bali kazi hii itakuwa endelevu kuanzia Mwezi Januari hadi Septemba. Mhe. Dendego ameyasema haya wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika kijiji cha Kalenga 08.12.2023.
“Sisi leo hatuna kilele tunasema ndio kwanza kazi imeanza, tunaendeleza hakuna kulala siku 360 zijazo lazima tuone matunda chanya kwa hiyo sisi hatufungi leo, Iringa kampeni hii ni endelevu” Amesema
Aidha, Mhe Dendego amesema mwendelezo wa kampeni hii utaambatana na mashindano juu ya kazi mbalimbali zinazolenga kupinga ukatili wa kijinsia. Mashindano hayo yatakayokuwa kwa ngazi mbalimbali kuanzia Tarafa, Wilaya na Mkoa ikihusisha makundi ya shule za Msingi, Sekondari, vyuo na makundi mengine katika jamii ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu atapata zawadi kwa kila ngazi.
Pia Mhe. Dendego metoa wito kwa jamii kuchukua tahadhari kufuatia mvua kubwa zinazonyesha katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa waangalifu juu ya watoto ili kuzuia au kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza na kuzitumia mvua hizi vema kwenye masuala ya kilimo.
Mhe. Dendego amewashukuru viongozi mbalimbali na wadau kutoka shirika la World Vision Tanzania, TAHEA, Emmanuel International, Care, FBF, Compassion International, Lebao’s Kids Foundation na wana Habari wote kwa kufanikisha Kampeni hii ya kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Mkoa amesema, mwaka jana Ukatili wa Kijinsia ulifikia 23% kwa Mkoa wa Iringa na watu wengi hasa wanaume wameanza kujitokeza kutoa taarifa za ukatili. Ameendelea kusema kuwa Chanzo kimojawapo kikubwa cha kuongeza ukatili ni mmomonyoko wa maadili katika jamii ambapo mmomonyoko huo umetokana na malezi mabaya katika familia.
Maadhimisho ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia mwaka huu yana ujumbe usemao, “Wekeza Kupinga Ukatili wa Kijisia”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa