Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wote wanaostahili kwenda shuleni wanaripoti na kuwaomba viongozi wote wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa vyama, viongozi wa taasisi, na jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kuwahimiza watoto waende wakaripoti shule.
Mhe. Kessy ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika Januari 25, 2024 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo – Iringa ambapo maada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo mchakato wa kugawa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
“Mpaka tarehe 31 watoto waripoti kwa hiyari, lakini kuanzia tarehe 01.02.2024 tutaanza msako unaanza kwa wazazi ambao hawajawaapeleka watoto wao shule. Na tumeshatoa maelekezo kwa Maafisa Elimu na Wakurugenzi watendaji kwamba tutahitaji orodha ya wanafunzi wote ambao walitakiwa kuanza kidato cha kwanza”.
Kwa upande mwingine kikao cha DCC kimeridhia kuendelea kwa mchakato wa kugawa Halmashauri ambapo mapendekezo ya awali ni kuwa na Halmashauri 2 yaani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruaha kutoka katika Halmashauri Mama ya Wilaya ya Iringa.
Inapendekezwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuchukua eneo lote la Jimbo la kalenga na Halmashauri ya Wilaya ya Raha kuchukua eneo lote la Jimbo la Isimani sanjari na mapendekezo ya ongezeko la mgawanyo wa kata, vijiji na vitongoji.
Akisoma taarifa ya mapendekezo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bi Beatrice Augustino Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu amesema mapendekezo hayo yamekuja kufuatia sababu ya kijiografia ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na mambo mengine.
Kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya kimefanya mapitio ya Mipango na Bajeti kwa mwaka 2023/2024 na rasimu ya 2024/2025 kwa Halmashauri ya wilayaya Iringa, Manispaa ya Iringa, Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali ikiwemo TANESCO, RUWASA, IRUWASA, TARURA, TANROADS, NIDA, LATRA na TRA.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa