IRNGA DC YAPATA GARI YA KISASA
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano Iringa –DC)
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw Robert Masunya amemshukuru Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu kwa kuipatia Halmashauri yake Gari ya Kisasa kwa ajili ya Kubebea Wagonjwa yenye thamani ya Shilingi Milioni 120.
“Namshukuru sana Waziri Mh Ummy Mwalimu kwa kuipa kipaumbele Halmashauri yetu ya Iringa kwani uwepo wa usafiri wa uhakika kutawezesha kuokoa maisha ya watu wengi inapokuwa imetokea dharura ya Mgonjwa kutaka kuwahishwa katika Hospitali ya Rufaa ”
Bw Masunya ametoa shukurani hizo Ofisini kwake Kalenga leo Mei 4 alipokuwa akipokea Gari hiyo na kutoa maelekezo kwa mkuu wa idara ya Usafirishaji Bw Hawadi Tom kuwa makini na kuhakikisha Gari hiyo inatunzwa kama ambavyo gari zingine zinatunzwa kwani hii ni Baraka kwa Halmashauri ya Wilaya Iringa.
“Gari hii itafanya Halmashauri yetu iwe na gari tisa,hivyo hakikisha hata dereva utakayemkabidhi ni dereva mstaarabu ambaye ataitumia kwa umakini na kwa weledi ili tuzidi kujenga imani kwa Serikali na wadau wotewanaojitolea misaada kwa ajili ya Halmashauri yetu” alisema.
Pia alitoa shukurani kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Wiliam Lukuvi, kwa kuisemea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizopewa magari ya kisasa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
“Upatikanaji wa Gari hii hata Mh Waziri William Lukuvi lazima ni mshukuru amekuwa akiguswa na kufuatilia masuala yote yahusuyo halmashauri awapo katika vikao vya Bunge mjini Dodoma”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa