World Vision yawakumbuka Watoto Wenye Ulemavu.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa DC)
Shirika lisilo la kiserlikali la World Vision limegharamia viti mwendo vyenye thamani ya shilingi million 24.9 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu katika Kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akizungumza baadha ya ugawaji wa viti hivyo mwezeshaji wa mradi huo Bi.Gaudencia Mushi amesema jumla ya watoto 43 walikuwa wamelengwa kupata viti hivyo lakini kabla ya kuanza kugawa waliwashilikisha wataalam wa mazoezi tiba kwa vitendo ili ugawaji huo usiweze kuleta madhara kwa wanufaika.
‘‘Si kila kiti mwendo kina faa kwa ajili ya watu wenye ulemavu au kila mtu mwenye mlemavu anatakiwa kupewa kiti mwendo hivyo sisi kabla ya kuanza kuwafikia watoto wenye walemavu tulishirikiana na wadau wenzetu kutoka hospitali ya CCBRT ambao wao ni wataalam wa mazoezi tiba kwa vitendo ’’ alisema na kuongeza;
“ Hivyo kati ya watoto 43 walioonwa ni watoto 29 ndio walikidhi vigezo na kupewa viti mwendo huku 14 wakipewa rufaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya katika hospitali za CCBRT Moshi,hosptali ya Machame na KCMC.”alisema.
Kwa upande wake Mtoa tiba kwa vitendo Bi.Neophita Lukilindi ametoa pongezi kwa Shirika la World Vision kwa kuwakumbuka watoto wenye ulemavu kwani wengi wa watoto hao wamekuwa hawatimizi ndoto zao.
Bi.Lukilindi alisema zoezi la ugawaji viti hivyo lilikuwa la siku nne na kwamba liligawanyika kikata ambapo tarehe 21 na 23 lilifanyika Kata ya Kihanga na tarehe 24 hadi tarehe 25 Kata ya Wasa ambapo maeneo hayo ndipo World Vision inafanya shughuli zake za kusaidia jamii.
“Napenda kuipongeza serikali yetu ya awamu ya tano kwa kuweza kuweka mazingira mazuri ambayo yanawezesha wataalam kufanya kazi kwa uhuru na amani eneo lolote ndani ya mipaka ya nchi yetu,lakini pia mahusiano mazuri kati ya serikali na mashirika na taasisi zisizo za kiserikali”alisema.
Aidha Bw.Marius John Muwakilishi wa shirika la World Vision Singida ambaye alikuwa msimamizi wa zoezi hilo amesema zoezi la utoaji wa viti hivyo umefanyika katika mikoa mitano ambayo shirika hilo lina miradi lakini pia wapo watoto ambao wamenufaika na ujio wa wataalam wa CCBRT kwani walipimwa kupewa ushauri na hata kupewa elimu ya kuwafanjia mazoezi watoto wao wawapo nyumbani.
“Wapo watoto ambao sio wafadhiliwa wa shirika na ambao hawapo eneo la Mradi lakini kwa kuwa walihitaji huduma za kitaalam waliweza kuonwa na kupewa vipimoikiwemo rufaa ili waweze kwenda kupata huduma za kiuchunguzi zaidi”alisema.
Bw.John alisisiza kwa kusema kuwa jamii inapaswa kushiriki katika kutetea na kulinda haki na maslahi ya watoto wenye ulemavu ili waweze kutimiza ndoto zao na kupata haki zao za kimsingi ikiwemo kusoma na kushiriki katika masuala ya kijamii.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa