Mwakilishi wa Ubalozi wa Japani Bi Nana Takeda ametembelea miradi iliyokuwa imejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya japani katika shule ya sekondari Idodi Februari 07, 2024. Miradi hiyo ni Bweni la wanafunzi linalochukua wanafuzi Zaidi ya 200 na mradi wa maji shuleni hapo ambao ni wa kisima kirefu kinachoendeshwa na pampu ya umeme.
Bi. Nana Takeda ameambatana na Afisa wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa afrika Mashariki Bi. Happiness Kimario. Lengo la ziara hii ni kufanya ufuatiliaji wa miradi yote ambayo imetekelezwa kwa ufadhili serikali ya Japani na kuona uendelevu wake sanjari na kutoa ushauri kwa kadri ya uhitaji.
Aidha ugeni huo kwa kushirikiana na viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa umeweza kutembelea Shule ya Msingi Mangalali na kijionea hali ya uchakavu wa vyumba vya madarasa ambapo wameahidi kujenga vyumba vitano vya madarasa kupitia shirika la RUDI.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa