MWENGE WA UHURU 2023 WAPOKELEWA MKOANI IRINGA KWA SHANGWE KUBWA
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Peres Boniface Magiri, amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Njombe.
Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthon Mtaka, Mhe. Magiri ameahidi kuutunza, kuulinda na kukimbizwa salama Mkoa mzima wa Iringa wenye Wilaya tatu na Halmashauri tano, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Halmashauri ya Mji Mafinga, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.
Akitoa salamu za Mkoa Mhe. Magiri amesema, “Mwenge utakimbizwa kwa jumla ya kilometa 719, na miradi ya Maendeleo 31 yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sitini na Tatu, Milioni Mia Moja Tisini na Nne, Laki Nane na Arobaini Elfu, Mia Tano na Ishirini na Saba na Senti Themanini na Nne (63,194,840,527.88).
Miradi hiyo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023 ni kwa ajili ya ufunguzi/uzinduzi, kuwekwa mawe ya msingi au kukaguliwa
Mwenge wa Uhuru 2023 Kauli mbiu yake inasema “Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Hifadhi ya Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa